Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI--MACHAR-SIASA

Riek Machar Kuapishwa Jumatatu

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatatu wiki ijayo jijini Juba.

Kiongozi wa upinzani na Makamu wa rais wa Sudan kusini Riek Machar, Julai 8, 2015.
Kiongozi wa upinzani na Makamu wa rais wa Sudan kusini Riek Machar, Julai 8, 2015. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Machar ataapishwa na rais Salva Kiir ambaye amekubali kushirikiana naye kuongoza serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Riek Machar anatarajiwa kuwasili jijini Juba siku ya Jumatatu na kuapishwa mara moja kwa mujibu wa msemaji wake, James Gatdet Dak.

Vikosi vya Machar vimekuwa vikisiwasili jijini Juba kwa maandalizi ya kumkaribisha Machar.

Katika hatua nyingine, rais Salva Kiir atakuwa mjini Arusha nchini Tanzania katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutia saini kwenye mkataba wa kujiunga na Jumuiya hiyo.

Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na Uganda, Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na sasa Sudan Kusini, ambayo ilikubaliwa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.