Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA-SHAMBULIO

Ufaransa yazima shambulio, watu wanne wakamatwa

Rais François Hollande amesema Jumatano, Julai 15 kwamba vitendo vya kigaidi vimezimwa wiki hii nchini Ufaransa. Watu wanne ambao walikuwa mpango wa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya mitambo ya kijeshi wamekamatwa, amesema Jumatano jioni waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi ulianzishwa wiki tatu zilizpita, wiki kuna tatu. Watuhumiwa, ikiwa ni pamoja na mwanajeshi mmoja wa zamani wa ikosi cha jeshi la majini wana umri kati ya miaka 16 hadi 23. Muungozaji mkuu wa shambulio hilo anajulikana kuwa na uhusiano na kundi la wanajihadi. Alikuwa akichunguzwa tangu mwishoni mwa mwaka 2014 kwa "harakati kwenye mitandao ya kijamii". Aliwahi kupewa "taarifa ya kusafiri nchini Syria". Wengine watatu yalijulikana baada ya kuwa kuwasiliana mara kadhaa na mtuhumiwa huyo. Kama watu walikamatwa katika maeneo tofauti nchini Ufaransa, ina maana kuwa wamekua wakiandaa jambo fulani, amesema waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa.

Hakuna uhusiano iwowote na tukio la moto lililotokea Jumanne wiki hii katika kiwanda kimoja mjini Berre l'Etang, amesema waziri wa mambo ya ndani.Ni wakati alipokuwa akijibu swali juu ya tukio la moto ambalo rais François Hollande, akiwa ziarani Marseille na rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, amesema mapema Jumatano mchana wiki hii kwamba mashambulizi yamezimwa wiki hii.

Idara za usalama nchini Ufaransa kwa sasa zimekuwa makini zaidi tangu kufanyika kwa mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya watu 17 katika mashambulizi yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.