Pata taarifa kuu
UN-UGANDA

Sam Kutesa rais mteule wa kikao cha baraza la Umoja wa Mataifa akanusha tuhma dhidi yake

Rais mpya mteule wa kikao cha baraza la Umoja wa mataifa UNGA, na pia waziri wa mambo ya kigeni wa Uganda, Sam Kutesa, amekanusha madai kuwa yeye ni mbaguzi na anashiriki vitendo vya rushwa nchini mwake, matamshi anayoyatoa saa chache baada ya kuteuliwa na nchi wanachama kuwa rais wa baraza hilo kwa mwaka mmoja.

Kushoto ni rais mteule wa kikao cha Umoja wa Mataifa Sam Kutesa na kulia ni Ban Ki Moon katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Kushoto ni rais mteule wa kikao cha Umoja wa Mataifa Sam Kutesa na kulia ni Ban Ki Moon katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa passblue.com
Matangazo ya kibiashara

Awali waziri Kutesa alikuwa anakabiliwa na upinzani mkali toka kwa baadhi ya wanachama wa Umoja huo ambao walimtuhumu kuwa anaongoza harakati za kibaguzi na kushiriki vitendo vya rushwa, tuhuma ambazo sasa kiongozi huyu anakanusha kwa nguvu na kudai kua zilikuwa njama za wapinzani wake.

Sam amesema: kwanza kabisa ningependa niwaambie haya, kwamba nimekuwa nikichafuliwa na viongozi wa upinzani kwenye nchini yangu, ndani na jje na mara zote wamekuwa wakijaribu kuharibu jina langu. Sijawahi kupatikana na hatia ya rushwa, mimi sio mbaguzi na naamini ni mtu sahihi kwenye taasisi hii kwa vikao vijavyo.

Kutesa amechaguliwa bila kupingwa na zaidi ya wajumbe 193, kwenye kura zilizopigwa siku ya Jumatano.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema Kutesa anauzowefu mkubwa, amekuwa wakili, mbunge, waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje na amemtakia kila la kheri katika majukumu yake kuongoza kiti hicho.

Punde baada ya kuchaguliwa, Sam Kutesa aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa yeye ni chaguo sahihi kwenye nafasi hiyo na kwamba atahakikisha anafanya kazi kwa viwango kutekeleza majukumu yake.

Ni lazima tueleze mbinu mpya za utekelezwaji, kifedha, kiteknologia na kujenga uwezo. haya yanahitaji ushirikiano wa kidunia. Lengo letu kubwa liwe ni kuleta ajenda za mabadiliko ambazo zitatoa suluhu ya matatizo, maendeleo na kuwezesha wananchi kujikwamua kuboresha maisha yaona kuamua mustakabali wa wa baadae.

Zaidi ya saini 13.200 zilikusanywa kuiomba Marekani ambako kunapatikana makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumyng'anya Visa kutokana na uungwaji wake mkono kuhusu sheria inayopinga ndoa ya watu wa jinsi moja iliopasishwa nchini Uganda hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.