Pata taarifa kuu
DR Congo

Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu wanakutana hii leo nchini Uganda kujadili usalama wa Congo

Viongozi kumi na mmoja kutoka nchi za Maziwa Makuu wanakutana hii leo Jijini Kampala nchini Uganda, kijadili hali ya Usalama katika eneo la Mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila
Matangazo ya kibiashara

Eneo la Mashariki mwa Congo limekuwa likikumbwa na Mashambulizi ya Waasi wa M23, ambalo wafuasi wake ni wapiganaji wa zamani wa kitutsi waliojiunga na Jeshi la nchi hiyo chini ya Mpango wa makubaliano ya Amani ya Mwaka 2009.

wakati kumekuwepo na hali ya utulivu katika eneo la Kivu ya Kaskazinitangu Mwezi Julai, bado hali ni tete Afisa kutoka Umoja wa Mataifa anayewakilisha katika eneo la Africa ya Kati Abou Mussa ameeleza

Ripoti ya Umoja wa Mataifa, iliishutumu Rwanda Mwezi June kwa kuwafadhili Waasi na kusababisha hali kuwa ya wasiwasi nchini Congo, shutma ambazo Kigali imezikana na imekuwa ikifanya Mazungumzo na Serikali ya Kinshasa kuhakikisha hali ya utulivu inarejea.

Mkutano wa hii leo unaohodhiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, utaangalia Mapendekezo yaliyotolewa na Mawaziri wa Ulinzi katika mkutano wao uliofanywa katikati ya mwezi jana Mjini Goma nchini DRC.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.