Pata taarifa kuu
TANZANIA

Serikali yaapa kuchunguza utekwaji nyara wa Dk. Ulimboka

Serikali ya Tanzania imekiri kushtushwa na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina kubaini wale ambao wamehusika kwenye utekwaji nyara na kumpiga Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Dokta Ulimboka Steven.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linaendelea na juhudi za kuwabaini wale ambao wamehusika kwenye utekaji na upigwaji wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dokta Ulimboka Steven.

Kauli ya Serikali inakuja wakati huu ambapo Wanaharakati wakiongozwa na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kupitia mkurugenzi wake Hellen Kijobi Simba wakitaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madaktari Dokta Edwin Chege amesema lengo la kumshambulia Mwenyekiti wao Dokta Ulimboka lilikuwa ni kukatisha uhai wake.

Sakata hilo linakuja wakati leo serikali iliahidi kutoa kauli yake na hatua ambayo itachukua kukabiliana na mgomo uliotangwaza na madkatari ambao umejiegemeza kwenye madai ya maslahi lakini kauli hiyo haitatolewa kwa sababu suala hilo liko mahakamani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dokta Emmanuel Nchimbi amesema kitendo hicho hakikubaliki dhidi ya raia yoyote yule na hivyo watahakikisha jeshi la polisi linatafuta na kupata ukweli wa tukio hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Madakatari nchini Tanzania, MAT Dokta Namala Mkopi amesema kitendo hicho cha kutekwa na kupigwa Dokta Ulimboka kinakatisha tamaa wanataaluma hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.