Pata taarifa kuu
EAC

Migomo ya walimu yatikisa Kenya, Uganda, Kongo

Walimu wa shule za msingi na zile za sekondari kutoka nchi za Kenya, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wamegoma kufundisha katika wiki ya kwanza baada ya shule kufunguliwa wakidai maslahi zaidi.

AP
Matangazo ya kibiashara

Nchini Kenya madai ya walimu hao ni kuitaka serikali kuajiri walimu elfu ishirini kutokana na uwepo wa uhaba wa walimu wakati nchini Uganda kikubwa ambacho kinadaiwa na walimu ni nyongeza ya mshahara.

Kiongozi wa Kamati Inayotetea Maslahi ya Walimu Mashariki mwa nchi hiyo ya DRC Baeni Ndalayitse Jeanluc ameeleza kuwa walimu nchini humo wenyewe hawataki kulipwa na wazazi huku wakiitaka serikali kuongeza.

Walimu wa Uganda halikadhalika wamegoma wakitaka nyongeza ya mishahara na maslahi zaidi ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha kutokana na kiwango kidogo cha mishahara kinacholipwa na Serikali.

Hali ya migomo imekuwa ikitumiwa kama nyenzo muhimu katika kudai haki za wafanyakazi wa umma na hata sekta binafsi katika nchi za Afrika Mashariki.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.