Pata taarifa kuu

Rwanda yawapokea wahamiaji kutoka nchini Libya

Nairobi – Nchi ya Rwanda, hapo jana ilipokea wahamiaji zaidi ya 90 kutoka Libya, chini ya mpango unaoungwa mkono na shirika la wakimbizi duniani UNHCR.

Wakimbizi hawa wanawasili huku ule mpango wa Uingereza na Kigali ubadilishana wahamiaji ukicheleweshwa kwa mara nyingine na bunge hadi baada ya sikukuu ya Pasaka
Wakimbizi hawa wanawasili huku ule mpango wa Uingereza na Kigali ubadilishana wahamiaji ukicheleweshwa kwa mara nyingine na bunge hadi baada ya sikukuu ya Pasaka © RBA
Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hawa wanawasili huku ule mpango wa Uingereza na Kigali ubadilishana wahamiaji ukicheleweshwa kwa mara nyingine na bunge hadi baada ya sikukuu ya Pasaka.

Kwa mujibu wa kiongozi wa shughuli za bunge Penny Mordaunt,mswada huo utakuwa shughuli ya Kwanza katika bunge la House of Commons baada ya likizo ya Pasaka.

Mswada huo ukipitisha unaorodhesha nchi ya Rwanda kuwa nchi salama kwa  wahamiaji na kutotumika baadhi ya vipengee vya sheria  vya haki za binadaam ili kukwepa vizingiti vya kisheria kutoka mahakama ambavyo vimeshuhudiwa kwa muda.

Bunge kuu  hivi majuzi lilikuwa limeangusha sheria hiyo likitaka serikali kuweka mikakati zaidi ya kuwalinda wakimbizi pia likitaka mabunge yote mawili kuafikiano kuhusu mswada huo.

Serikali ya waziri mkuu Rishi Sunak,ilipanga  kuwapa hifadhi nchini Rwanda, wahamiaji  wanaowasili nchi hiyo kila mwaka kutumia boti ,ila mahakama imeendelea kuuzuia mpango huo ikiituhumu Kigali kwa kutoheshimu haki za binadaam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.