Pata taarifa kuu

Wabunge wa EAC wanakutana jijini Nairobi kwa kikao maalum

Nairobi – Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanakutana jijini Nairobi, katika kikao maalum, ambapo imekubalika kuwa nchi wanachama watamuunga mkono mgombea mmoja kuwania Unyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. fr.wikipedia.org
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kenya William Ruto akifungua kikao hicho, ambacho kwa mara ya kwanza kimehudhuriwa na wabunge kutoka DRC, amesema mwafaka umepatikana kati ya marais wenzake kumuunga mkono mgombea mmoja, kumrithi Mouusa Faki atakapoachia wadhifa huo mwaka ujao.

00:15

Rais Ruto kuhusu mgombea wa AUC

Kenya imewasilisha jina na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kuwania wadhifa huo, huku Somalia ikisema Waziri wake wa zamani wa Mambo ya nje Fawzia Adam atawania nafasi hiyo.

Mbali na suala hilo, Ruto amesasihi wabunge hao kujadiliana kuhusu ubaguzi kutoka kwa mashirika ya Kimataifa kuhusu fedha, zinazotolewa kwa nchi za Afrika.

00:21

Rais Ruto kuhusu mikopo na akiba

Matamshi sawa yakitolewa na spika wa bunge hilo.

00:13

Spika wa bunge la EALA

Wabunge hao wametoa wito kwa nchi wanachama kuchangia kwa uaminifuada ya Jumuiya hiyo ili kufanikisha miradi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.