Pata taarifa kuu

Kenya: Wabunge wapitisha marekebisho ya muswada kuhusu nyumba za bei nafuu

Nairobi – Katika kile kinachoonekana kuelekea kupata ushindi mwingine kisiasa, wabunge nchini Kenya, wamepitisha marekebisho ya muswada wa sharia kuhusu nyumba za bei nafuu ili uendane na uamuzi uliotolewa na mahakama ambayo ilizuia utekelezwaji wake.

Baadhi ya raia wa Kenya wamekuwa wakipinga mpango huo wa serikali wakati wengine wakiuunga mkono.
Baadhi ya raia wa Kenya wamekuwa wakipinga mpango huo wa serikali wakati wengine wakiuunga mkono. Β© William Ruto
Matangazo ya kibiashara

Baada ya uamuzi wa wabunge, muswada huo sasa utapelekwa kwenye bunge la seneti kujadiliwa, ambako wadadisi wa mambo wanasema hawatarajii kuona ukipingwa au kubadilishwa.

Kwa hatua hii, inmaanisha kuwa wakenya walioajiriwa wataanza kukatwa tena asilimia 1.5 ya mishahara yao kufadhili mpango huo.

Kupitishwa kwa muswada huu katika bunge, kumekuwa pigo kwa upinzani ambapo licha ya wabunge wake zaidi ya 20 kuupinga, ulipitishwa na wabunge wengi wanaomuunga mkono rais William Ruto.

Utawala wa rais William Ruto unasema kuwa mpango huo unalenga kutoa ajira kwa vijana wengi ambao hawana ajira.
Utawala wa rais William Ruto unasema kuwa mpango huo unalenga kutoa ajira kwa vijana wengi ambao hawana ajira. Β© William Ruto

Muswada huo ulitupiliwa mbali na mahakama kwa kile ambacho waliofungua kesi wanasema sharia hiyo ni yakibaguzi na kinyume cha katiba.

Serikali ya rais William Ruto imekuwa ikitetea mpango huo ikisema kwamba unalenga kutoa ajira kwa idadi kubwa ya vijana ambao hawana ajira kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mpango huo aidha umeonekana kuwagawa baadhi ya raia nchini humo, wengine wikuunga mkono wakati wengine wakiuupinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.