Pata taarifa kuu

Kenya: Raia watoa heshima za mwisho kwa Kelvin Kiptum, katika mkesha wa mazishi ya kitaifa

Mamia ya watu wametoa heshomaza mwisho siku ya Alhamisi kwa Kelvin Kiptum, mshindi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za wanaume za Kenya aliyefariki katika ajali ya gari siku kumi na moja zilizopita, katika ajali ya barabarani huko Eldoret, nchini Kenya. Alifariki pamoja na kocha wake, Gervais Hakizimana, raia wa Rwanda. 

neza la mwanariadha wa mbio za marathon wa Kenya Kelvin Kiptum linaonekana karibu na picha ya ukumbusho wakati wa mazishi yake katika kijiji cha Chepkorio, Februari 22, 2024.
neza la mwanariadha wa mbio za marathon wa Kenya Kelvin Kiptum linaonekana karibu na picha ya ukumbusho wakati wa mazishi yake katika kijiji cha Chepkorio, Februari 22, 2024. © LUIS TATO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Likisindikizwa na nyimbo, au kwa ukimya, jeneza, lililozungukwa na maua, kwa matumaini makubwa ya wanariadha wa Kenya lilisafiri kwa gari la kubebea maiti wakati wa msafara katika mitaa ya Eldoret, eneo maalumu kwa ajili ya mbio za miguu. Baba na mamake wa mwanariadha huyo, Samson Cheruiyot na Mary Kangongo, walifika wakilia karibu na jeneza, kabla ya msafara kuanza.

Jeneza la Kiptum lilielekea Iten, kituo maarufu cha mafunzo kwa wanariadha wa masafa marefu na wa masafa ya kati. Kisha misa iliadhimishwa huko Chepkorio, takriban kilomita arobaini kutoka Eldoret.

Kelvin Kiptum, mshindi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za wanaume za Kenya, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 24, alikuwa na mke na alikuwa baba wa watoto wawili, atazikwa Ijumaa kwa "mazishi ya kitaifa", mbele ya Rais William Ruto, yatakayofanyika Naiberi. "Hili ni pengo kubwa katika riadha ya Kenya na itachukua muda kulijaza," mkuu wa programu ya vijana katika Shirikisho la Riadha la Kenya, Barnaba Korir, ameliambia shirika la habari la AFP.

Saa mbili na sekunde 35

Kulingana na daktari wa uchunguzi, Kelvin Kiptum, ambaye uchunguzi wake wa madai ya sumu bado unaendelea, alifariki kufuatia majeraha mabaya kichwani. Akichukuliwa kuwa nyota anayechipukia wa riadha wa Kenya na ulimwengu, Kelvin Kiptum aliingia kwa kishindo katika ulimwengu wa mbio za marathoni kwa kuvunja rekodi ya dunia (dakika 2 h 00) katika mbio zake rasmi za tatu, mjini Chicago mwezi Oktoba mwaka jana akivunja rekodi ya dunia iliyokuwa ikishikiliwa na Eliud Kipchoge, pia raia wa Kenya.

Kiptum alianza kukimbia mara kwa mara mwaka wa 2016. Mnamo 2019, aliweza kukimbia mbio za nusu marathoni kwa kasi sana katika muda wa wiki mbili (60:48 Copenhagen kisha 59:53 Belfort, Ufaransa), wakati Gervais Hakizimana alipojitolea kumfundisha kwa marathon, ushirikiano wao ukizima wakati wa janga la UVIKO-19 mnamo mwaka 2020.

Kiptum mara kwa mara alikimbia zaidi ya kilomita 250 kwa wiki, na wakati mwingine zaidi ya 300, takwimu adimu hata katika kiwango cha juu sana, alibaini mkufunzi wake, Mnyarwanda Gervais Hakizimana, mkazi wa Ufaransa, mkimbiaji wa ngazi ya taifa ambaye alikutana na Kiptum wakati wa ziara yake ya mafunzo nchini Kenya. Hakizimana alizikwa nchini Rwanda siku ya Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.