Kenya: Watu wawili wamefariki katika mlipuko wa gesi, 222 wajeruhiwa
Nairobi – Karibia watu wawili wamethibitishwa kufariki katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi nchini Kenya, wakati wengine karibia 222 wakiendelea kupokea matibabu baada ya kutokea mlipuko mkubwa wa gesi usiku wa kuamkia leo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Picha zilizonaswa kwenye eneo la tukio zimeonyesha nyumba, biashara na magari yakiwa yameharibiwa vibaya moto mkubwa ukiwaka karibu na majengo ya ghorofa.
Two people killed, 222 injured after an explosion at a gas refilling company in Embakasi, Nairobi. pic.twitter.com/Ekn5w46Bfl
— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) February 2, 2024
Inadaiwa kuwa huenda moto huo ulisababishwa na mlipuko uliotokea kwenye lori la kusafirisha mitungi ya gesi licha ya hapo awali msemaji wa serikali ya Kenya kudai kuwa mlipuko huo ulitokea katika kiwanda cha gesi.
Licha ya taarifa hizo za kukinazana kuhusu chanzo cha mlipuko huo, mashahidi wanadai kuwa chanzo kilikuwa ni kiwanda kinachodaiwa kujishugulisha na biashara ya mitungi ya gesi.
“It was a disaster in waiting,” Embakasi resident reacts after a gas explosion that has so far left three people dead pic.twitter.com/cLleBe9FOY
— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) February 2, 2024
Hapo awali, shirika la msalaba mwekundu la Kenya lilikuwa limeripoti karibu watu 300 waliojeruhiwa.
Moto huo ulizuka Alhamisi usiku katika kitongoji cha Embakasi kusini mashariki mwa mji mkuu.Wakaazi wengi wa eneo hilo walilala nje usiku kucha.
Polisi wamezingira eneo lililoathiriwa, lakini baadhi ya watu walionekana wakikusanya mali zao na kuchunguza uharibifu huo.
Mnamo 2018, moto katika soko la Gikomba jijini Nairobi uliua watu 15 na kujeruhi takriban 70.
Mamlaka kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki kwa sasa inaendelea kuchunguza kubaini chanzo halisi cha mlipuko huo wa usiku wa kuamkia leo.
Car on the rooftop, twisted metal, melted plastic, cracked buildings... devastation after gas explosion in Embakasi pic.twitter.com/VASl8KAU9d
— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) February 2, 2024