Pata taarifa kuu

Fahali aliyemuua mchungaji wake auawa Mgaharibi ya Kenya

Nairobi – Nchini Kenya, fahali anayemilikiwa na seneta  wa jimbo la Kakamega Magharibi ya taifa hilo la Afrika Mashariki, hapo jana Jumapili amemuua mchungaji wake.

Mashindano ya kuwapiganisha mafahali ni maarufu Magahribi ya Kenya
Mashindano ya kuwapiganisha mafahali ni maarufu Magahribi ya Kenya ASSOCIATED PRESS - Daniel Ochoa de Olza
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Seneta Boni Khalwale, mmiliki wa fahali huyo maarufu kama Inasio, aliripotiwa kumuua Kizito Moi, ambaye amekuwa akimtunza pamoja na fahali wengine kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20.

Mwili  wa mchungaji huyo ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa kichwani, shingoni, tumboni na mgongoni asubuhi ya Jumapili iliopita.

Kulingana na tamaduni za kabila la waluyha anakotokea Seneta huyo,  fahali huyo aliuawa  na kisha  nyama yake  kugawanywa baina ya wanakijiji.

Fahali huyo mwenye umri wa miaka mitano, aliyekuwa na uzani wa kilo 120, alikuwa ametawazwa hivi majuzi kuwa bingwa wa mashindano ya kupiganisha mafahali, mchezo maarufu Magharibi ya Kenya.

Seneta ni miongoni mwa watu maarufu ambao wamekuwa wakiandaa mashindano ya kuwapiganaisha mafahali, shughuli ya kitamaduni inayoenziwa na wengi haswa katika kaunti ya Kakamega.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.