Pata taarifa kuu

DRC: Wanasiasa wa upinzani wamesema hawatapinga matokeo ya uchaguzi

Nairobi – Wanasiasa wakuu wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamesema hawatawasilisha madai ya kupinga ushindi wa rais Félix Tshisekedi. 

Muda wa kuwasilisha rufa ya kupinga ushindi huo mahakamani unakamilika siku ya Jumatano
Muda wa kuwasilisha rufa ya kupinga ushindi huo mahakamani unakamilika siku ya Jumatano © Pascal Mulegwa / RFI
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi kwenye taifa hilo CENI, tarehe 31 ya mwezi Desemba ya mwaka wa 2023 ilimtangaza rais Tshisekedi mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata asilimia 73 ya kura zote, akifuatia na mfanyibiashara Moïse Katumbi, aliyepata asilimia 18. 

Moïse Katumbi, aliibuka watatu katika uchaguzi huo wa mwezi Desemba
Moïse Katumbi, aliibuka watatu katika uchaguzi huo wa mwezi Desemba AFP - ALEXIS HUGUET

Aliyekuwa gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga na mfanyabiashara mashuhuri Moise Katumbi, Martin Fayulu aliyeibuka wa tatu na mshindi wa Tuzo la amani la Nobel mwaka 2018 Dkt Denis Mukwege ni miongoni mwa wagombea urais ambao kambi zao zinasema hawatapinga ushindi huo katika mahakama ya katiba.   

Muda wa kuwasilisha rufa ya kupinga ushindi huo mahakamani unakamilika siku ya Jumatano. 

Wanasiasa hao wa upinzani wanadai kuwa uchaguzi huo haukufanyika kwa haki
Wanasiasa hao wa upinzani wanadai kuwa uchaguzi huo haukufanyika kwa haki © Pascal Mulegwa / RFI

Iwapo hakutakuwa na pingamizi dhidi ya ushindi huo, katika muda wa siku saba, rais Tshisekedi ataapishwa tarehe 20 ya mwezi Januari. Uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto za usafiri na za kiufundi. 

Tayari chama cha rais wa zamani nchini DRC,Joseph Kabila, PPRD ambacho hakikushiriki chaguzi zilizofayika nchini humo, ambapo tangu mwanzo wa mchakato kilisusia kwa kudaikuwa hakuna uaminifu na tume ya uchaguzi pamoja na mahakama ya kikatiba kimeendelea kushinikiza kuanzishwa upya mchakato wa uchaguzi.

Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila
Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila AP - John Bompengo
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.