Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Burundi washtumiwa kwa ubakaji nchini DRC

Wanajeshi wa Burundi waliotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) "waliwabaka na kuwatesa raia wa Kongo", shirika lisilo la kiserikali la haki za binadamu nchini Burundi limeshtumu siku ya Ijumaa, likiomba mamlaka kufanya "uchunguzi wa kuaminika".

Wanajeshi wa Burundi wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Machi 5, 2023.
Wanajeshi wa Burundi wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Machi 5, 2023. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

"Tangu mwisho wa mwaka 2021, wanajeshi wa Burundi (...) wamebaka na kuwatesa raia wa DRC huko Kivu Kusini", mashariki mwa DRC, limesema shirika la Haki za Kibinadamu nchini Burundi la IDHB, likidai kuwa vitendio hivyo vilifanywa "kwa siri, bila uangalizi wowote au uwajibikaji wowote".

Makundi mengi yenye silaha na wanamgambo wengine wameendelea na ukatili wao kwa miongo mitatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, urithi wa vita vya kikanda vilivyozuka katika miaka ya 1990 na 2000. Kwa miaka kadhaa, jeshi la Burundi limekuwa likifanya operesheni ya pamoja na vikosi vya Kongo Mashariki mwa nchi.

shirika hili la Haki za Kibinadamu nchini Burundi, mnamo Septemba 2022 "askari wa Burundi walimbaka mwanamke wa Kongo na shemeji yake mwenye umri wa miaka 16, mbele ya watoto wake watatu". IDBH pia imeshutumu vuguvugu la vijana wa chama tawala nchini Burundi, Imbonerakure, kwa "kuteka nyara, kuwaweka kizuizini kiholela na kuwatesa raia wa Kongo, na kupora mali zao."

IDBH inasema "wadau wa kimataifa" wanapaswa kuweka shinikizo kwa mamlaka ya Burundi, hasa Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, "ili kuwawajibisha wanajeshi wao". Rais Évariste Ndayishimiye, Waziri wa Ulinzi wa Burundi Alain Tribert Mutabazi pamoja na mwenzake wa DRC Jean-Pierre Bemba, hawakujibu maombi ya shirika hili lisilo la kiserikali.

Ikiwa jumuiya ya kimataifa imekaribisha ufunguzi fulani wa nchi tangu kuingia madarakani kwa Evariste Ndayishimiye mnamo mwezi Juni 2020 baada ya kifo cha ghafla cha Pierre Nkurunziza, tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha mnamo Septemba 2021 kwamba hali ya haki za binadamu bado ni "mbaya" nchini Burundi.

Mamia kadhaa ya wanajeshi wa Burundi kutoka kikosi cha Afrika Mashariki kilichotumwa mashariki mwa DRC waliondoka katika eneo hilo siku ya Jumapili, baada ya kutorejeshwa kwa misheni yake na Kinshasa ambayo ilionekana kushindwa kutekeleza majukumu yake. Lakini wanajeshi wa Burundi bado wapo ndani ya mfumo wa makubaliano ya nchi mbili.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.