Pata taarifa kuu

Bintou: Mvutano kati ya DRC na Rwanda unaongeza hatari ya makabiliano ya Kijeshi

Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, Bintou Keita, ameelezea wasiwasi wake kuhusu tishio la mapigano kati ya nchi hiyo na nchi jirani ya Rwanda.

Bintou Keita, mkuu wa tume ya MONUSCO akiwa mbele ya baraza la usalama, Disemba 11, 2023.
Bintou Keita, mkuu wa tume ya MONUSCO akiwa mbele ya baraza la usalama, Disemba 11, 2023. © @UNPeacekeeping
Matangazo ya kibiashara

Kwenye ripoti yake kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Keita amesema hali hii inaongeza hatari ya makabiliano ya kijeshi ambayo yanaweza yakaenea hadi nchi ya Burundi.

Kiongozi huyo wa MONUSCO ameliambia baraza hilo kuwa majimbo ya mashariki ya DRC, yanakabiliwa na ukosefu wa usalama unaoongezeka, hasa ​​kuhusiana na mzozo mpya wa M23.

Ripoti iliyo mbele yenu inaeleza namna hali ilivyo kwa sasa, pamoja na hatua zilizopigwa katika mchakato wa uchaguzi. Pia ina ainisha kuendelea kuzorota kwa usalama kwenye eneo la Mashariki na hasa uasi mpya ulioanzishwa na kundi la M23 lakini pia uwezekano wa kutokea mapigano katika ameneo mengine ya nchi, hasa eneo la Katanga na majimbo ya Mai-Ndombe na Tshopo

Onyo lake lilikuja muda mfupi tu baada ya mabalozi kutoka nchi hizo mbili kulaumiana wakiwa mbele ya baraza hilo, wakati huu pia ikiwa ni siku chache tu kabla ya uchaguzi wa Disemba 20.

Balozi wa DRC, Zenon Mukongo, aliwashutumu wanajeshi wa Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, akitaja matukio yaliyoanza Novemba 2022, akisisitiza wito wa nchi yake, wa kukomesha uchokozi wa Rwanda, kuondolewa kwa wanajeshi wake na kukomeshwa kwa makundi yenye silaha nchini Kongo, kadhalika kulitaka Baraza la Usalama kuchukua hatua kufanikisha hili.

Kwa upande wake balozi wa Rwanda kwa Umoja wa Mataifa, Ernest Rwamucyo, ameishutumu serikali ya DRC, makundi yenye silaha na mamluki wa kigeni kwa kukiuka mchakato wa amani wa kikanda na kuitaka serikali kujitolea tena kwa makubaliano hayo.

Kauli yake pia inajiri katika kipindi hiki vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki vinaondoka nchini humo lakini pia vikosi vya MONUSCO kutakiwa kuondoka kufikia mwishoni mwa mwaka huu wakidai kushindwa kuwalinda raia, badaa ya kuwa nchini humo kwa zaidi ya miongo miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.