Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini DRC: Waangalizi kutoka EU waelekea kujiondoa?

Nairobi – Zikiwa zimesalia siku kadhaa ili kufanyika uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tarehe 20 mwezi desemba 2023, ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umefahamisha kuwa bado haujapewa vibali vyote vinavyohitajika vinavyowaruhusu kutumia vifaa vyake vya mawasiliano nchini DRC.  

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umefahamisha kuwa bado haujapewa vibali vyote vinavyohitajika vinavyowaruhusu kutumia vifaa vyake vya mawasiliano nchini DRC.
Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umefahamisha kuwa bado haujapewa vibali vyote vinavyohitajika vinavyowaruhusu kutumia vifaa vyake vya mawasiliano nchini DRC. © Paulina Zidi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maafisa wakuu wanaowakilisha nchi za umoja huo wa ulaya nchini humo, ni kuwa hali inazidi kuwa mbaya, ikizingatiwa kuwa muda wa kufanyika kwa uchaguzi huo umeonekana kuwa umekaribia wakati ujumbe huo wa waangalizi wa Umoja wa ulaya umeshindwa kuanza kuzifanya shughuli zake; na sasa ujumbe huo umetishia kujiondoa katika nchi hiyo. 

Vyanzo kadhaa vya kidiplomasia vya Ulaya vimethibitisha kwamba majadiliano yanaendelea: "Hakuna jambo ambalo limeamuliwa kwa njia moja au nyingine, lakini kuna shida kubwa, amekiri mwanadiplomasia mmoja aliyeko Kinshasa na ambaye aliomba jina lake libanwe. 

Majadiliano yanayofanyika kati ya Kinshasa na Brussels ndio yatakayoamua kuhusu mustakabali wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya kuwepo nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, baada ya kuhakikishiwa iwapo uchaguzi wa mwaka huu utaahirishwa au la. 

Zimeenea fununu za kuahirishwa kwa uchaguzi huo, katika mitandao ya kijamii, baadhi wakidai kwamba tume ya Uchaguzi CENI haijadhihirisha kuwa tayari kukamilisha zoezi hili la Uchaguzi huku kukiwa na taarifa kwamba kiasi fulani cha pesa kinahitajika kutoka kwa serikali ya Kinshasa, na ambacho bado hakijatolewa. 

Kufikia Novemba 17, karibu waangalizi arobaini waliotakiwa kukaa kwa muda mrefu hadi kufanyika kwa uchaguzi wa DRC walitumia siku chache katika mafunzo Kwenye mji mkuu, Kinshasa, na baadaye walitakiwa kusafiri hadi kwenye mikoa 17 kati ya 26 ya nchi hiyo, huku Umoja wa ulaya ukiwa umepanga kuwatuma watu  karibu mia moja nchini kufuatilia uchaguzi huo wa desemba 2023. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.