Pata taarifa kuu

Kenya : Mfalme wa Uingereza kutamatisha ziara yake ya siku nne

Nairobi – Mfalme wa Uingereza, Charles wa tatu anatarajiwa kutamatisha ziara yake nchini Kenya kwa kukutana na viongozi wa dini katika jiji la Pwani la Mombasa, ambalo amekuwa akizuru kuanzia hapo jana.

Kiongozi huyo pia alikutana na baadhi ya wapigania uhuru na ndugu zao na kuzuru makaburi ya mashujaa wa uhuruoctobre 2023.
Kiongozi huyo pia alikutana na baadhi ya wapigania uhuru na ndugu zao na kuzuru makaburi ya mashujaa wa uhuruoctobre 2023. AP - Luis Tato
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya mkutano huo, Mfalme Charles atatembelea Kanisa Kuu la Angilikana, na baadaye kukutana na viongozi hao wa dini kujadiliana nao kuhusu kazi zao za kuimarisha amani, usalama na maendeleo, Pwani ya nchi hiyo.

Jana, Mfalme huyo alizuru kambi ya wanajeshi wa majini ya Mtongwe, kujionea mafunzo yaliyotolewa na wanajeshi wa Uingereza kwa wenzao wa Kenya, kuhusu namna ya kupambana na adui majini.

Malema pia amemkashifu rais Ruto kwa kutomshinikiza mfalme wa Uingereza kuzungumzia dhuluma za wakati wa ukoloni
Malema pia amemkashifu rais Ruto kwa kutomshinikiza mfalme wa Uingereza kuzungumzia dhuluma za wakati wa ukoloni REUTERS - PHIL NOBLE

Kabla ya kwenda Mombasa, Mfalme Charles alizuru jiji kuu Nairobi kwa siku mbili na kukiri madhila yaliyofanywa na serikali za kikoloni, lakini hakuomba msamaha licha ya kupokea shinikizo kutoka kwa wanaharakati mbalimbali.

Hata hivyo, alikutana na baadhi ya wapigania uhuru na ndugu zao na kuzuru makaburi ya mashujaa wa uhuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.