Pata taarifa kuu

DRC: Washirika wa Kabila watoa masharti kuhusu uchaguzi mkuu

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jukwaa la kisiasa linalomuunga mkono rais wa zamani wa Joseph Kabila, limesisitiza masharti yake mbele ya wajumbe wa Jumuiya ya SADC, ili kushiriki uchaguzi wa Desemba 20 mwaka huu.

Rais wa zamani wa DRC  Joseph Kabila
Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila Kenny Katombe/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwishoni mwa juma lililopita ujumbe wa SADC umekuwa ukikutana na wakuu wa vyama vya siasa pamoja na wajumbe wa tume ya uchaguzi nchini DRC, lengo likiwa ni kutathmini maandalizi na mchakato wa uchaguzi, baada ya kuenea uvumi kuwa CENI inakabiliwa na changamoto.

Miongoni mwa maafisa wa vyama vya siasa waliokutana na ujumbe huo ni pamoja na jukwaa la kisiasa linalomuunga mkono rais wa zamani Joseph Kabila, FCC, ambalo bila ya kung’ata maneno, limetoa masharti ili kushiriki uchaguzi huo.

Miongoni mwa masharti waliyotoa ni pamoja na kutaka uwakilishi wa upinzani ndani ya tume ya uchaguzi, CENI, Kubuniwa kwa mahakama ya kikatiba yenye uwiano na iliyo huru, kutangazwa kwa sheria ya uchaguzi inayokubalika na pande zote, usalama wa wanasiasa wa upinzani na kurejeshwa kwa hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa nchi na pia katika jimbo la Mai-Ndombe.

Wadadisi wa mambo bado wanaendelea kutilia shaka kufanyika kwa uchaguzi wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na shida za usalama, katika maeneo kadhaa ya mashariki mwa taifa hilo kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.