Pata taarifa kuu

DRC: Rais Tshisekedi apunguza hali ya dharura mashariki ya nchi

Nairobi – Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Felix Tshisekedi ametangaza usiku huu hatua za kupunguza hali ya dharura katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri mashariki mwa nchi hiyo, miaka miwili na miezi sita baada ya majimbo hayo kushuhudia kufuatia ongezeko la mauaji na usalama mdogo unaosababishwa na makundi yenye silaha.

Hatua hii ya kipekee iinakuja miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu, ukiwemo ule wa urais
Hatua hii ya kipekee iinakuja miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu, ukiwemo ule wa urais AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya kipekee iinakuja miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu, ukiwemo ule wa urais, itarahisisha kurejelewa tena kwa mikutano ya kisiasa, utawala wa kiraia na kupunguzwa kwa doria. 

Vital Kamerhe ni mshirika wa karibu wa rais wa DRC Felix Tshisekedi katika muungano watakatifu.
Vital Kamerhe ni mshirika wa karibu wa rais wa DRC Felix Tshisekedi katika muungano watakatifu. AFP - ALEXIS HUGUET

Rais Felix Tshisekedi anasema ameamua kupunguza taratibu hali hii ya dharura kwa awamu, ambapo kwanza itakuwa kurejesha polepole mamlaka ya kiraia kwenye majimbo ambayo tayari yanadhibitiwa na majeshi yetu na yanashuhudia usalama ikimaanisha sasa kutakuwa na uhuru wa kikatiba wa wananchi wote na kwa namna ya kipekee kusitishwa kwa doria. 

“Katika kuchukua kipimo cha sahidi kuhusu kurejeshwa kwa usalama wa raia wetu, kurejeshwa kwa maisha ya kiraia lakini pia katika kutambua maendeleo chanya ya utawala wa hali ya dharura.” amesema rais Felix Tshisekedi.

00:35

Mkuu wa nchi ya DRC kuhusu hali ya dharura

Hali ya dharura ilitangazwa mnamo Mei 3, 2021 kufuatia amri ya rais ili kukomesha utovu wa usalama unaojirudia katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

 

Wanajeshi wa Afrika Mashariki na wale ya serikali ya DRC wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi
Wanajeshi wa Afrika Mashariki na wale ya serikali ya DRC wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi AFP - ALEXIS HUGUET

 

Hivi karibuni rais Tshisekedi aliitisha mkutano wa wadau mbali mabli wakiwemo wabunge, wawakilishi wa mashirika ya kiraia kutaka kupata maoni yao kuhusu kusitishwa ama kuendelea kwa hali hiyo, lakini kukawa na mgawanyiko mkubwa, baadhi wakisema kuendelea kwa ukosefu wa usalama hakuruhusu kusimamisha hali hiyo, huku sauti nyingi zikitoa wito wa kuondolewa kwa hali hiyo na utawala wa kijeshi kwa kuwa haikuzaa matunda. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.