Pata taarifa kuu

DRC : Waliohusika na mauaji ya raia zaidi ya 50 mjini Goma wahukumiwa

Nairobi – Mahakama ya kijeshi nchini DRC, imemuhukumu adhabu ya kifo afisa mmoja wa juu katika jeshi pamoja na kifungo cha miaka 10 jela kwa maofisa wengine watatu, baada ya kuwakuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya raia zaidi ya 50 mjini Goma, Agosti 30 mwaka huu.

Hukumu dhidi ya askari hawa, imepokelewa kwa hisia na ahueni kwa familia ambazo zilipoteza ndugu zao 57 wakati wa maandamano
Hukumu dhidi ya askari hawa, imepokelewa kwa hisia na ahueni kwa familia ambazo zilipoteza ndugu zao 57 wakati wa maandamano AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hii ni ya juu zaidi kutolewa katika taifa ambalo sio mara zote limekuwa likishuhudia kutolewa kwa adhabu kama hizi, ambapo haijawahi kutekelezwa kwa zaidi ya miaka 20 na hugeuzwa kuwa kifungo cha maisha.

Mawakili wa wanajeshi hao hata hivyo wamesema watakata rufaa kupinga uamuzi huo, huku askari wengine wawili waliokuwa kwenye kesi hiyo, wakifutiwa mashtaka.

Licha ya mwendesha mashtaka wa serikali siku ya ijumaa wakati akifunga hoja zake kutoiitisha adhabu ya juu dhidi ya Kanali Mike Mikombe, majaji wameona adhabu hiyo inafaa huku wakimuondolea mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Hukumu dhidi ya askari hawa, imepokelewa kwa hisia na ahueni kwa familia ambazo zilipoteza ndugu zao 57 wakati wa maandamano yaliyokuwa yameitishwa kupinga uwepo wa vikosi vya umoja wa Mataifa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.