Pata taarifa kuu

DRC yafungua ubalozi wake mdogo Mombasa Kenya

Nairobi – Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imefungua ubalozi mdogo katika mji wa pwani ya Kenya Mombasa, hatua inayokuja siku chache baada ya nchi hizi kuondoa Visa kwa watu wanaosafiri kuwatembelea ndugu zao kwenye nchi hizi mbili wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Hatua hii inakuja baada ya Kenya kufungua ubalozi wake mdogo mjini Lubumbashi mkoani Haut Katanga kusini mashariki mwa Congo.   
Hatua hii inakuja baada ya Kenya kufungua ubalozi wake mdogo mjini Lubumbashi mkoani Haut Katanga kusini mashariki mwa Congo.    AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa ofisi hiyo ndogo huko Mombasa, Balozi wa DRC Nyakeru John Kalunga amesema kuwa lengo ni kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na DRC lakini pia kuwarahisishia wafanyabiashara wa kigeni pamoja na watu wengine kupata huduma zinazotolewa ubalozini. 

Kambale Mukokoma Eliphaz ndiye ameteuliwa kuwa mkuu wa ubalozi mdogo huko Mombasa, ameishukuru serikali ya Kinshasa kwa kuchukua mpango wa kuufungua ubalozi huo mdogo hapo Mombasa akiwataka wafanyabiashara walioko eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuanza kuwekeza katika nchi ya Kenya na kushirikiana nao katika kukuza sekta ya biashara wakati huu nchi hizi zote mbili zimeamua kuondoa visa. 

‘‘Sisi kwetu ni kuweza kuishukuru serikali ya DRC kwa kuweza kufungua afisi hii katika eneo la Mombasa, tunaishukuru pia serikali ya Kenya.’’ alisema Kambale Mukokoma Eliphaz.

00:55

Kambale Mukokoma Eliphaz, kuhusu ubalozi wa mdogo wa DRC Mombasa Kenya

Hatua hii inakuja baada ya Kenya kufungua ubalozi wake mdogo mjini Lubumbashi mkoani Haut Katanga kusini mashariki mwa Congo.   

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.