Pata taarifa kuu

DRC: Jenerali Smith Bihanga ameshtakiwa baada ya kukamatwa jijini Kinshasa

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kiongozi wa jeshi katika mkoa wa kijeshi wa Lubumbashi Jenerali Smith Bihanga ameshtakiwa baada ya kukamatwa jijini Kinshasa, kwa wizi wa tani 120 ya shaba yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 1.2 kutoka kampuni ya madini ya TFM.

kiongozi wa jeshi katika mkoa wa kijeshi wa Lubumbashi Jenerali Smith Bihanga ameshtakiwa baada ya kukamatwa jijini Kinshasa
kiongozi wa jeshi katika mkoa wa kijeshi wa Lubumbashi Jenerali Smith Bihanga ameshtakiwa baada ya kukamatwa jijini Kinshasa RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na jeshi, Jenerali Smith Bihanga, aliyetajwa katika kashfa ya wizi wa tani 120 za shaba alitakiwa kujiwasilisha Jumatano ya wiki hii katika afisi za idara ya upelelezi ya kijeshi huko Kinshasa kabla ya kuzuiliwa.

Taasisi ya utafiti wa haki za binadamu, IRDH ambayo iliwasilisha malalamiko kuhusu kesi hii, inataka ukweli kuwekwa wazi kuhusu kinachoendelea. Hubert Tshwaka, mkurugenzi wa IRDH.

“Tunafuraha kwa sababu Jenerali Smith hatimaye atafikishwa mahakamani. Kwa hivyo tunaweza kupata majibu kwa maswali yetu yote. ” alisema Hubert Tshwaka, mkurugenzi wa IRDH.

00:17

Hubert Tshwaka, mkurugenzi wa IRDH

Jenerali Smith Bihanga aliondolewa madarakani kama kamanda wa mkoa wa 22 wa kijeshi.

Viongozi wa wakuu wa jeshi walifanya mabadiliko mengine upande wa mahakama ya kijeshi mjini Lubumbashi. Kanali Bashonga amechukua nafasi ya kanali Lita kama mkaguzi mkuu. 

Denise Maheho, Lubumbashi, RFI Kiswahili 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.