Pata taarifa kuu

DRC: Mkutano kuhusu hali ya dharura Ituri na Kivu Kaskazini umetamatika

Nairobi – Nchini DRC, hakuna uamuzi uliotangazwa baada ya majadiliano ya wadau kuhusu hali ya dharura iliyowekwa kwenye majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini, ingawa kwa sehemu kubwa wanasiasa kutoka kwenye maeno hayo wanataka amri hiyo kuondolewa.

Raïs Tshisekedi anasubiriwa kuchukua uamuzi wa mwisho kuhusu kuondolewa kwa hali ya dharura
Raïs Tshisekedi anasubiriwa kuchukua uamuzi wa mwisho kuhusu kuondolewa kwa hali ya dharura AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Bila kuzungumzia kama hali ya dharura imeondolewa ndani ya jimbo la Kivu-Kaskazini na Ituri, waziri Mkuu wa DRC Sama Lukonde, alitamatisha mkutano huu wa siku 3.

‘‘Natangaza kutamatika kwa mazungumzo haya kuhusu hali ya dharura katika jimbo la Ituri na Kivu Kaskazini, ripoti hii itatolewa kwa raia wa Kongo.’’ alisema Sama Lukonde.

00:15

Sama Lukonde, Waziri mkuu wa DRC

Katika mazungumzo haya asilimia 80 ya tume ambazo zilikuwa zimeunda kundi za washiriki, walikuwa wametaka raïs Tshisekedi kuondoa hali ya dharura katika majimbo hayo.

Jacques Sinzahera, ni mwanaharakati wakundi la amka kongo

‘‘Mkuu wa nchi mwenyewe anafahamu kwamba maoni ya raia wa maeneo hayo mawili ya Kivu Kaskazini na Ituri wanataka kuondolewa kwa hali ya dharura.’’ alisema Jacques Sinzahera, ni mwanaharakati wakundi la amka kongo.

00:10

Jacques Sinzahera, ni mwanaharakati wakundi la amka kongo

Kundi lingine la wabunge lilitaka hali ya dharura isiondolewe kutokana na vitisho vya makundi ya watu wenye silaha kwenye maeneo hayo kama anavyoeleza Adelard Minene.

‘‘Vitu ambayo vilifanya raïs atangaze mpango wa dharura ni usalama mdogo huko kwetu, na hiyo hali bado ipo hadi sasa.’’ alielezaAdelard Minene.

00:12

Adelard Minene kuhusu hali ya dharura DRC

Kwa sasa raïs Tshisekedi anasubiriwa kuchukua uamuzi wa mwisho kuhusu kuondolewa kwa hali ya dharura kwa mujibiu wa Sama Lukonde waziri Mkuu wa DRC.

Freddy Tendilonge/ Kinshasa/ RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.