Pata taarifa kuu

Fulgence Kayishema, amekamatwa tena nchini Afrika Kusini

Nairobi – Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Fulgence Kayishema, ambaye amekuwa akizuiliwa nchini Afrika Kusini, amekamatwa tena kwa mujibu wa amri inayomtaka kusafirishwa hadi Arusha, Tanzania, kufunguliwa mashtaka ya mauji ya halaiki.

Nchini Rwanda, anatuhumiwa kuwa na jukumu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994
Nchini Rwanda, anatuhumiwa kuwa na jukumu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994 REUTERS - NIC BOTHMA
Matangazo ya kibiashara

Fulgence alikamatwa wakati akiwa katika seli za mahakama kuu mjini Cape Town mapema Jumanne.

Mahakama hiyo inamtaka ajibu mashtaka ambapo anadaiwa kuwa  alipanga mauaji ya takriban wakimbizi 2,000 wa Kitutsi katika kanisa katoliki nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Kayishema tayari yuko kizuizini nchini Afrika Kusini ambapo alikamatwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo.

Wachunguzi wa Afrika Kusini walisema amekuwa akiishi Afrika Kusini chini ya jina la uongo tangu kuwasili kwake mwaka 2000.

Nchini Rwanda, anatuhumiwa kuwa na jukumu muhimu katika mauaji ya kimbari ya 1994, kushiriki katika mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wakati alipofikishwa mahakamani mara ya mwisho mwezi Juni, aliondoa  ombi lake la dhamana na kusema kwamba angeomba hadhi ya ukimbizi nchini Afrika Kusini.

Kesi dhidi yake imeahirishwa hadi Agosti 30 ili kuruhusu mawakili wake na waendesha mashtaka wa eneo hilo kujibu amri ya kukamatwa na kuhamishiwa kwengine.

Hajakubali rasmi mashtaka dhidi yake, lakini hapo awali amekana kuhusika katika uhalifu huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.