Pata taarifa kuu

DRC: Wadau waeleza kutoridhishwa na maandalizi kuekekea uchaguzi mkuu

Nairobi – Kanisa Katoliki na mashirika ya kiraia nchini DRC, yameeleza Kutoridhishwa kwao na matayarisho ya nchi hiyo kuelekea uchaguzi wa mwezi Disemaba mwaka huu.

Kanisa Katoliki na mashirika ya kiraia nchini DRC, yameeleza Kutoridhishwa kwao na matayarisho ya nchi hiyo kuelekea uchaguzi wa mwezi Disemaba mwaka huu.
Kanisa Katoliki na mashirika ya kiraia nchini DRC, yameeleza Kutoridhishwa kwao na matayarisho ya nchi hiyo kuelekea uchaguzi wa mwezi Disemaba mwaka huu. Daniel Finnan
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa mashirika hayo ni kwamba matayarisho ya uchaguzi wa mwezi Disemba hayaridhishi kutokana na kwamba yanakubwa na mizozo kwenye ngazi zote, na hilo halitowi picha nzuri ya kuleta amani baada ya uchaguzi kufanyika.

Rais wa bazara la maskofu wa kanisa katoliki Jean-Bosco Lalo amesema hakuna hakikisho kutoka kwa serikali kuhusiana na swala la usalama kwa kuwalinda raia kuelekea uchaguzi huo na hata baaada ya uchaguzi, akiongeza kuwa uwepo wa makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakitekeleza uhalifu nchini humo, kuuawa kwa mwanaisiasa Chérubin Okende, ni ishara tosha kuwa raia wa DRC hawana usalama kuelekea uchaguzi huo na baada ya uchaguzi.

Mashirika hayo yameongeza kuwa hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu nchini DRC, imesalia ya taharuki, viongozi walio madarakani wakikosa kuaminiana, na pia kukosoa hatua ya serikali kutumia nguvu kupita kiasi kuwakabili wandamanajai na idara ya mahakama kutumika kuwakandamiza wapinzani.

Aidha  mashirika pia yamekosoa hali ya uchumi wa DRC yakihusisha hali hiyo na uongozi mbaya ambao umechangia kuporomoka kwa uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.