Pata taarifa kuu

Watu wanne wamefariki katika ajali ya moto kwenye soko la Ngaba DRC

Nairobi – Juma hili katika jiji la Kinshasa nchini DRC, ajali ya moto katika soko moja lenye idadi kubwa ya watu ilisababisha vifo vya watu wanne, baada ya lori la mafuta kulipuka.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Ngaba, soko lenye shughuli nyingi katika wilaya ya Lemba kusini mwa jiji kuu.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Ngaba, soko lenye shughuli nyingi katika wilaya ya Lemba kusini mwa jiji kuu. CIA world factbook
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na runinga ya kitaifa, watu sita ndo walifariki, huku naibu wa gavana wa jiji la Kinshasa, Gérard Lumumba, ambaye alifikkwenye eneo la ajali, akieleza kuwa ni watu 5 ndiyo walipoteza maisha.

‘‘Nimeagiza meya wa mkoa aweze kubomoa nyumba zote zilizo jengwa kando ya barabara, nyumba hizo ndiyo zimesababisha madhara zaidi baada ya lori kugonga magari mengine.’’ alisema Gérard Lumumba, naibu gavana wa Kinshasa.

00:14

Gérard Lumumba, Naibu gavana wa Kinshasa

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Ngaba, soko lenye shughuli nyingi katika wilaya ya Lemba kusini mwa jiji kuu.

Moto huo ulisababishwa na lori la kusafirisha mafuta kuharibika breki zake na kugonga nguzo ya umeme.

Nyumba kadhaa za biashara ziliteketea katika ajali kama anavyoeleza mmoja wa waathiriwa.

‘‘Tumepoteza bidhaa zetu, nyumba kuungua na watu kadhaa wamefariki.’’

Visa vya ajali mara nyingi huripotiwa katika masoko ya Kinshasa.

Freddy Tendilonge- RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.