Pata taarifa kuu

DRC: Matata Ponyo atangaza azma yake ya kuwania urais

Nairobi – Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Augustin Matata Ponyo, ametangaza kuwa atawania urais, wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 20.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Augustin Matata Mponyo
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Augustin Matata Mponyo © Frederico Scoppa, AFP
Matangazo ya kibiashara

Matata Mponyo, anaugana na wanasiasa wengine kama Moise Katumbi, ambaye pia ameonesha nia ya kuwania urais kupambana na rais Felix Tshisekedi.

Ametoa tangazo hilo akiwa mjini Kindu, alipokutana na wafuasi wake na kueleza ni kwa nini anataka kuongoza nchi hiyo.

“Tuna mpango kabambe wa kurekebisha serikali na kuifanya kuwa ya kisasa ilikuifanya iwe na ufanisi wa kuishindani na lazima tujenge jeshi bora na jeshi la polisi lenye ufanisi na kuwa na ujerani mwema.” alisema Matata Ponyo.

00:21

Matata Mponyo kuhusu siasa za DRC

Kuhusu mpango wake anaosema ni wa kuifanya nchi ya DRC kutimiza ndoto zake Matata Ponyo anaamini anasema anaamini Kongo imara ambayo kila raia ana uhuru na nyenzo za kufanya kazi kwa mafanikio yake na taifa.

Aidha mwanasiasa huyo anasema maono yake ni kuitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka katika kundi la nchi maskini zaidi duniani ndani ya miaka 5, na kuipandisha kwenye daraja la nchi zenye uchumi wa kati.

Aidha mwanasiasa huyo anasema maono yake ni kuitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka katika kundi la nchi maskini zaidi duniani ndani ya miaka 5
Aidha mwanasiasa huyo anasema maono yake ni kuitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka katika kundi la nchi maskini zaidi duniani ndani ya miaka 5 AFP / Junior D. Kannah

Kwake yeye, ni lengo shupavu, dhabiti ambalo linaweza kufikiwa kwa uongozi wa fikra, dhamira thabiti, mkakati uliobainishwa vyema, malengo na vitendo mahususi vinavyoweza kupimika na ufuatiliaji na tathmini madhubuti.

Haya yanajiri wakati huu tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO ikisema itachunguza kifo cha mwanasiasa wa upinzani Cherubin Okende, aliyepatikana ameuawa jijini Kinshasa, Julai 13.

Jenerali Mody Berethe anayehusika na masuala ya kipolisi , ameteuliwa kuongoza uchunguzi huo.

“Polisi na wataalam wanaofuatilia shughuli hiyo, watafanya kazi chini ya mamlaka ya vyombo vya sheria, timu ya wachunguzi wetu itajiunga na wataalam wengine ambao wako tayari.” alisema Jenerali Mody Bereth.

 

00:36

Jenerali Mody Berethe

 

Aidha Mody ameeleza kuwa upande wa DRC kuna timu tatu na mchango wao kama MONUSCO utakuwa wa kiufundi kulingana na maarifa walio nayo kama polisi stadi wenye taaluma ya kisayansi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.