Pata taarifa kuu

Wapemba nchini Kenya kupewa vitambulisho vya kitaifa

Nairobi – Nchini Kenya rais William Ruto leo anatarajiwa kuwakabidhi vitambulisho vya taifa na hati ya kusafiria watu wa kabila jipya la wapemba ambao wamekuwa wakiishi kwa miongo kadhaa Pwani ya nchi hiyo bila kutambuliwa kama raia. 

Wapemba kwa muda sasa wamekuwa wakihangaika kwa kukosa vitambulisho vya kitaifa nchini kenya
Wapemba kwa muda sasa wamekuwa wakihangaika kwa kukosa vitambulisho vya kitaifa nchini kenya © Namati -Kenya
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda, hiki kimekuwa ni kilio kutoka kwa jamii ya wapemba ambayo ina watu zaidi ya elfu saba  

Tulipozungumza na Mwalimu Ali Mkasha katibu mwenezi wa jamii ya Wapemba êneo la Kichaka Mkwaju miezi mitatu iliyopita, alikuwa na kumbukumbu zenye uchungu. 

“Huwa tunanunua wazazi hata watato, sehemu nyengine unalipishwa ama upate jirani mwema akuambie wewe ni ndugu yangu.” alisimulia Mwalimu Ali Mkasha katibu mwenezi wa jamii ya Wapemba.

00:08

Mwalimu Ali Mkasha katibu mwenezi wa jamii ya Wapemba

Leo hii hata hivyo kilio hicho kimebadilika na kuwa wimbo mpya wanavyosema viongozi hao kutoka jamii hiyo. 

“Watu ambao tumejitokeza kuwa Wapemba ni watu zaidi ya elfu saba lakini kuna wenzetu wengine ambao hawakujitokeza wakati tunapopambana kupata uraia kwamba tutafungwa, tunaomba serikali iweze kutupa nafasi ya kutafuta vitambulisho vingine.” alisema mmoja wa viongozi wa Wapemba.

00:18

Mmoja wa viongozi wa Wapemba

Ukurasa huu mpya umefunguliwa kutokana na juhudi za wanajamii na wanaharakati wa haki za binadaam. Lawrence Lore ni afisa kutoka shirika la Haki Centre 

‘‘Tuliweza kuwasaidia kwa kuwapa kadi ya uanachama ili kila moja mmoja awe nayo kumtambulisha kama mmoja wa Wapemba ilikumsaidia anaposhikiwa na polisi.’’ alieleza Lawrence Lore ni afisa kutoka shirika la Haki Centre 

00:10

Lawrence Lore ni afisa kutoka shirika la Haki Centre

Mwaka 2020 bunge la Kitaifa, lilipitisha pendekezo la kuitambua jamii ya Wapemba kama raia wa Kenya, hatua aliyoidhinisha rais mwezi Februari mwaka huu. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.