Pata taarifa kuu

Kenya: Asilimia 52 ya raia hawana imani na serikali: Utafiti

Nairobi – Utafiti wa shirika la TIFA, umeonesha kuwa asilimia 52 ya wakenya hawana imani na serikali ya rais William Ruto kutokana na kuendelea kupanda kwa gharama ya maisha.  

Rais wa Kenya William Ruto alitia saini muswada wa fedha 2023 kuwa sheria
Rais wa Kenya William Ruto alitia saini muswada wa fedha 2023 kuwa sheria © Statehouse Kenya
Matangazo ya kibiashara

Aidha, utafiti huo umeonesha kuwa kwa kipindi cha miezi 10 iliyopita, raia wa nchi hiyo ambao ni sawa na asilimia 51, wanaamini kuwa kiongozi wao hajatekeleza ahadi alizozitoa. 

Asilimia 56 ya wakenya katika utafiti huo wanasema kwamba taifa hilo linaelekea pabaya wakati asilimia 25 ikisema kwamba nchi inaelekea pahali pazuri.

Raia katika taifa hilo la Afrika wamekuwa wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha wakitaka serikali kuangazia suala hilo ambalo wanasema limekuwa changamoto kwa raia wa chini.

Upinzani nchini humo ukiongozwa na Raila Odinga, umekuwa ukiwaongoza wafuasi wao kuaandamana kupinga kile wanachosema ni serikali ya rais William Ruto kutoshugulikia suala hilo la mfumuko wa bei za bidhaa.

Micheal Mwarenge ni mkuu wa utafiti katika shirika la TIFA.  

“Maisha yamekuwa magumu haswa baada ya bei ya mafuta kupanda, bei za bidhaa zinazidi kuongezeka pia hatua ambayo raia wametuambia kwamba serikali haielekei katika mwendo mzuri.” alisema Micheal Mwarenge ni mkuu wa utafiti katika shirika la TIFA.

00:29

Micheal Mwarenge ni mkuu wa utafiti katika shirika la TIFA

Serikali ya Kenya, imekuwa ikitupilia mbali tafiti za mashirika kama haya, ikisema hazina ukweli wowote. 

Rais Ruto ameteta uamuzi wa serikali kuongeza ushuru kwa baadhi za petroli akisema kwamba hatua hiyo inalenga kulisaidia taifa lake kulipa madeni kwa wakopeshaji wake wa kimataifa.

Kando na kuongezwa kwa ushuru wa bidhaa hizo za petroli, serikali nchini humo inawataka raia wake kuchangia asilimia 1.5 ya mapato yao kuelekea kwa hazina ya kitaifa inayolenga kuwajengea raia makazi bora, mpango ambao umesitishwa na mahakama kwa muda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.