Pata taarifa kuu

DRC: Hali ya usalama ni tishio kwa uchaguzi mkuu: Wadau

Wadau wa uchaguzi nchini DRC, wanasema uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka huu, unatishiwa na hali ya uotvu wa usalama katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa nchi hiyo, wakiitaka Serikali kuimarisha usalama kwenye maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Dénis Kadima, amewahakishia raia wa DRC uchaguzi wa huru na wa haki
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Dénis Kadima, amewahakishia raia wa DRC uchaguzi wa huru na wa haki © CENI DRC
Matangazo ya kibiashara

Makundi yenye silaha yamekuwa yakitatiza usalama katika eneo la mashariki wakati huu kukiripotiwa matukio ya utekaji nyara jijini Kinshasa, hali ambayo wadau hao wameitaka serikali kushugulikia kwa haraka.

Kando na suala la usalama, vyama vya kisiasa, mashirika ya kiraia na wawakilishi wa mahakama ya kikatiba walizungumzia kuhusu hatari ya taarifa za uongo, za kupotosha na matamshi ya uchochezi kuelekea uchaguzi huo.

Masuala ya matamshi ya chuki na uchochezi kwa misingi ya kikabila yametajwa kuwa kizingiti katika maandalizi ya uchaguzi huo na hatima yake.

Rais wa tume ya uchaguzi nchi DR Congo Denis Kadima kwa upande wake amekuwa akitoa hakikisho ya kufanyika kwa uchaguzi wa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.