Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Watano wauawa, baadhi wakatwa vichwa, katika shambulio la Al Shabab mashariki mwa Kenya

Raia watano waliuawa, na baadhi kukatwa vichwa, katika shambulio la Jumamosi jioni katika vijiji viwili mashariki mwa Kenya, shambulio ambalo limedaiwa na wanamgamo wa Kiislamu wenye itikadi kali wa Al Shabab, kulingana na vyanzo vya polisi na wakaazi siku ya Jumapili.

Askari wa jeshi la Kenya katika ulinzi mkali kwenye kaunti la Lamu pwani ya Kenya January 2 2020.
Askari wa jeshi la Kenya katika ulinzi mkali kwenye kaunti la Lamu pwani ya Kenya January 2 2020. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitekelezwa mwendo wa saa moja na nusu usiku saa siku ya Jumamosi saa za Kenya katika vijiji vya Juhudi na Salama, vilivyoko katika kaunti ya pwani ya Lamu, inayopakana na Somalia, kulingana na vyanzo hivi. "Watu watano waliuawa (...) Wahanga walikatwa vichwa na kuna wengine waliuawa kikatili," chanzo cha polisi kmeliambia shirika la habari la AFP.

Mmoja wa waliouwawa ni mwanamume mwenye miaka sitini ambaye alifungwa kamba na kisha kukatwa koo na nyumba yake ikateketezwa. Watu wengine wa tatu waliuwawa kwa namna hiyo hiyo huku mtu wa tano akiuwawa kwa kupigwa risasi.

Taarifa ya polisi nchini humo imesema washambuliaji hao pia walichoma nyumba na kufanya uharibifu wa mali katika tukio iliyoliita kuwa ni la kigaidi na baadaye walikimbilia msituni.

Kaunti ya Lamu inapatikana karibu na mpaka wa Somalia na wapiganaji wa al Shabab, wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa kuishinikiza serikali ya Kenya iwaondoe wanajeshi wake nchini Somalia, ambao ni sehemu ya vikosi vya kulinda amani vya kimataifa vinavyoilinda serikali dhaifu ya Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.