Pata taarifa kuu

DRC :Serikali kufanya tathmini ya hali ya dharura maeneo ya Kivu Kaskazini na Ituri

NAIROBI – Serikali ya DRC imesema kwamba Kazi za maandalizi ya mkutano unaotathmini maendeleo ya hali ya dharura kwenye majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, zinaendelea Vizuri jijini Kinshasa, na kwamba wadau wa kitaifa na wa kimataifa watashiriki mazungumzo hayo.

Makundi ya watu wenye silaha yamekuwa yakiwatatiza raia katika eneo la Ituri Mashariki ya DRC
Makundi ya watu wenye silaha yamekuwa yakiwatatiza raia katika eneo la Ituri Mashariki ya DRC AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Katika taaifa yake kwa Vyombo vya habari ofisi ya waziri Mkuu imefahamisha kuwa kuanzia leo juni 20 mazungumzo yanayolenga kutathmini hali ya dharura inayoendelea kwenye majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini.

Nini matarajio ya raia wa eneo hilo? Wakili David Bwambale ni mwanaharakati wa huko Beni.

“Tangu zamani tulikuwa tunasubiri tathmini kuhusu hali ya dharura ambayo inapaswa kufanyika kwa hali ya ukweli.” alisema Wakili David Bwambale, mwanaharakati wa huko Beni.

00:12

Wakili David Bwambale ni mwanaharakati wa huko Beni

 

Raia wengi wameona kuwa hali hiyo imeshindwa kuzaa matunda kama anavyoeleza Peguy Matsipa akiwa Goma,

“Tulikuwa na matumaini kwamba ni swala ambalo linaweza kutusaidia ila hali inaendelea kuharibika siku baada ya siku.” alieleza  Peguy Matsipa akiwa Goma.

00:13

Peguy Matsipa, Mkaazi wa Goma

 

Haya yanajiri wakati watu wanne wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio la kuvizia kwenye barabara inayounganisha Kitshanga-Mweso.Heritier Ndange Ndange ni mtaalamu wa usalama huko Goma.

“Ni vigumu sana kutambua ni nani aliyewajeruhi hawa watu na kupora mali yao, eneo hili lipo katika barabara inayolindwa na wanajeshi wa EAC.” alieleza Heritier Ndange, Mtaalamu wa usalama huko Goma.

00:15

Heritier Ndange Ndange ni mtaalamu wa usalama huko Goma

 

Hali ya dharura iliyoanzishwa tangu Mei 6, mwaka 2021 katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri kwa lengo la kuimarisha usalama, imekuwa ikikosolewa na mashirika ya kiraia ambayo yamesema haijazaa matunda yoyote, na badala yake kasi ya mauaji imeongezeka kwenye majimbo hayo kufuatia mashambulio ya waasi wa ADF, na makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.