Pata taarifa kuu

Sudan: RSF yalaani mauaji ya gavana wa  Darfur

NAIROBI – Wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, wamelaani kuawawa kwa gavana wa jimbo la Darfur Magharibi Khamis Abbakar siku ya Jumatano ya wiki hii.

Mohamed Hamdan Dagalo, Kiongozi wa RSF
Mohamed Hamdan Dagalo, Kiongozi wa RSF REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Awali maofisa wa serikali ya Sudan walikuwa wamewatuhumu wapiganaji wa RSF kwa kutekeleza mauaji ya gavana  ambaye kabala ya kifo chake alikuwa amewatuhumu wapiganaji hao na makundi mengine yenye silaha kwa kuhusika na mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa kabila la Masalit.

RSF kupitia ujumbe wake kwenye ukurasa wa twitter inasema gavana huyo aliwauawa na makundi mawili ya kihalifu licha ya vikosi vyake kujaribu kumlinda.

“Makundi ya kihalifu yalitekeleza shambulio kwenye makazi hali ambayo haingeweza kudhibitiwa kutokana na idadi kubwa ya wahalifu hao ambao walimteka gavana huyo kabla ya kumuuwa” RSF imeeleza katika taarifa yake.

Kundi hilo limetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi uliosababisha kifo chake na kusema kwamba litachukua hatua iwapo mmoja wa maofisa wake atahusishwa katika tukio hilo la mauaji.

Kifo cha gavana huyo kinakuja huku kukiwa na ongezeko la mashambulio ya  kikabila na ukatili dhidi ya raia katika eneo la Darfur, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.