Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Maafisa wanane wa polisi wa Kenya wauawa katika mlipuko unaohusishwa na Al Shabab

Maafisa wanane wa polisi wa Kenya wameuawa wakati gari lao lilipoharibiwa na kilipuzi katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na Waislam wenye itikadi kali wa Al-Shabab wanaoishi nchini Somalia, polisi imesema.

Maeneo jirani na Somalia yamekuwa yakikabiliwa na tishio la wapiganaji wa Al-Shabaab
Maeneo jirani na Somalia yamekuwa yakikabiliwa na tishio la wapiganaji wa Al-Shabaab ASSOCIATED PRESS - Mohamed Sheikh Nor
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lilitokea siku ya Jumanne katika kaunti ya Garissa mashariki mwa Kenya, eneo linalopakana na Somalia, ambapo Al-Shabab wanaendesha uasi wa umwagaji damu dhidi ya serikali dhaifu ya Mogadishu kwa zaidi ya miaka 15.

"Tulipoteza maafisa wanane wa polisi katika shambulio hili," Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki John Otieno amesema. "Tunashuku" "al Shabab ambao sasa wanalenga vikosi vya usalama na magari ya abiria," ameongeza.

Jeshi la Kenya liliingilia kati mwaka wa 2011 nchini Somalia kupambana na al Shabab. Vikosi vyake vilijiunga mwaka 2012 na kikosi cha Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia (AMISOM, ambayo kwa sasa inaitwa ATMIS), ambacho kiliwatimua Al Shabab kutoka katika ngome zao kadhaa.

Tangu mwaka 2011, Kenya imekuwa mlengwa wa mashambulizi kadhaa mabaya yaliyodaiwa na Al Shabab, hasa dhidi ya kituo cha ubiashara cha Westgate huko Nairobi (Septemba 2013, watu 67 waliuawa), Chuo Kikuu cha Garissa (Aprili 2015, watu 148 waliuawa) na hoteli ya Dusit ( Januari 2019, watu 21 waliuawa).

Mashambulizi mengine mengi madogo huwalenga maafisa wa polisi na raia karibu na mpaka. Nchini Somalia, Al-Shabaab wameendelea na mashambulizi yao mabaya licha ya mashambulizi makubwa yaliyoanzishwa mwezi Agosti mwaka uliyopita na vikosi vinavyounga mkono serikali, vikisaidiwa na kikosi cha AU (ATMIS.

Katika mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi ya hivi majuzi, walinda amani 54 wa Uganda waliuawa wakati Al-Shabab walipovamia kambi ya AU nchini Somalia Mei 26, kulingana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Siku ya Jumamosi, raia sita waliuawa wakati wa uvamizi wa Al-Shabab katika hoteli iliyo ufukweni mwa Mogadishu, kulingana na polisi ya Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.