Pata taarifa kuu
DINI-USALAMA

Kenya: Idadi ya waliofariki kutokana na 'mauaji ya Shakahola' yazidi 300

Idadi ya vifo vya 'mauaji ya Shakahola', yaliyopewa jina la msitu mmoja nchini Kenya ambapo dhehebu la kiinjili linalotetea mfungo uliokithiri lilikutana, imeongezeka hadi watu 303 siku ya Jumanne, miezi miwili baada ya kufichuliwa kwa kisa hiki  ambacho kiliikashifu nchi hii ya Afrika Mashariki.

Zoezi la upasuaji wa miili ya waliofariki wakifunga kula chakula nchini Kenya linaendelea
Zoezi la upasuaji wa miili ya waliofariki wakifunga kula chakula nchini Kenya linaendelea © REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

"Idadi ya waliofariki sasa imeongezeka hadi 303 baada ya kufukuliwa kwa miili 19," gavana wa Mkoa wa Pwani Rhoda Onyancha amesema siku ya Jumanne. Ripoti hii bado ni ya muda na mamlaka ya nchi hii ya Afrika Mashariki inahofia kuwa itakuwa nzito zaidi.

Zoezi la kutafuta makaburi ya halaiki bado linaendelea katika Msitu wa Shakahola, eneo la msituni karibu na mji wa pwani wa Malindi, ambapo waathiriwa wa kwanza - baadhi walifariki, wengine wakiwa hai lakini wamedhoofika kiafya - waligunduliwa Aprili 13. Tangu wakati huo, msururu wa uvumbuzi wa miili umefichua kashfa mbaya, iliyopewa jina la "Mauaji ya Msitu wa Shakahola".

Uchunguzi umepanuliwa zaidi ya hekta 325 za awali hadi sasa kufikia karibu hekta 15,000. Zaidi ya watu 600 wametangazwa kutoweka na ndugu zao waliokuwa na wasiwasi. Polisi inaamini kwamba miili mingi iliyofukuliwa ni ya waumini wa Kanisa la Kimataifa la Habari Njema (Good News International Church), dhehebu la kiinjili lililoundwa mwaka wa 2003 na mtu anayejiita "mchungaji" Paul Nthenge Mackenzie, ambaye alitetea kufunga hadi kifo ili "kukutana na Yesu (Isa)".

Akiwa kizuizini tangu ajisalimishe kwa polisi Aprili 14, dereva huyu wa zamani wa teksi mwenye umri wa miaka 50 anashitakiwa kwa "ugaidi".

Watuhumiwa walionusurika

Uchunguzi wa maiti ulizofanywa kufikia sasa umefichua kuwa wengi wa waathiriwa walikufa kwa njaa, huenda baada ya kufuata mahubiri ya Paul Nthenge Mackenzie. Lakini pia uchunguzi ulibaini kwamba baadhi ya wahanga wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa au kukosa hewa.

Rais William Ruto, mwenyewe Mprotestanti shupavu aliyeungwa mkono na waumini wengi wa kiinjilisti alipochaguliwa Agosti 2022, aliunda jopokazi "kukagua mfumo wa kisheria na udhibiti unaoongoza mashirika ya kidini". Majaribio ya hapo awali ya kudhibiti yamekabiliwa na upinzani mkali, hasa kwa jina la uhuru wa kuabudu.

Mamlaka zitaufanya Msitu wa Shakahola kuwa "mahali pa ukumbusho", Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alitangaza wiki jana, "ili Wakenya na ulimwengu wasisahau kilichotokea".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.