Pata taarifa kuu

Raia 10 wa DRC wameuawa katika mapigano nchini Sudan

NAIROBI – Raia 10 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepoteza maisha nchini Sudan kufuatia vita vinavyoendelea kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF.

Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Sudan licha ya wito wa jamii ya kimataifa ya kutaka kusitishwa kwa vita
Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Sudan licha ya wito wa jamii ya kimataifa ya kutaka kusitishwa kwa vita AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kinshasa inasema raia wake waliuawa baada ya jeshi la Sudan kutekeleza mashambulio ndani ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Afrika, jijini Khartoum.

Mapigano yanayoendela nchini Sudan kwa wiki ya nane na raia hao wa DRC ni miongoni mwa watu 1800 waliopoteza maisha tangu kuanza kwa vita hivyo, wakati huu mazungumzo kati ya pande hasimu, yakikwama.

Naibu waziri mkuu anayehusika na mambo ya nje nchini DRC Christophe Lutundula amemsikiliza jana muhusika wa maswala ya mambo nje katika ubalozi wa Sudan Jijini Kinshasa kupata maelezo zaidi kuhusu vifo vya wanafunzi 10 raia wa Congo waliouawa na mabomu yaliorushwa na vikosi vya serikali katika chuo kimoja nchini Sudan.

Christophe Lutundula amebaini maskitiko yake kuona jeshi la serikali ndilo linalohusika.

“Tumemuomba mhusika kwenye ubalozi kutupa maelezo ya kina, kama mnavyojuwa ni jeshi la serikali ndilo ambalo lilihusika na kushambulia chuo, tumeitaka serikali kuhakikisha miili inakabidhiwa na kurejeshwa.”alisema Christophe Lutundula.

00:49

Christophe Lutundula kuhusu Sudan

Waziri huyo amesema serikali inasubiri mamlaka ya Sudan kutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo.

Khartoum inakabiliwa na mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa (RSF) tangu Aprili 15, huku raia wakinaswa katika mapigano hayo.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetoa wito wa kuwepo kwa korido ya kibinadamu ili kuiwezesha kuwaondoa raia wake waliojeruhiwa na wengine ambao bado wamekwama mjini Khartoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.