Pata taarifa kuu

Kenya: Bei ya mafuta yapanda tena

NAIROBI – Wakenya kuanzia Jumatatu wameanza kulipia bei ya juu wanaponunua bidhaa za petroli kufuatia tangazo la bei mpya iliyotangazwa na mamlaka inayodhibiti bidhaa hiyo (EPRA).  

Bei ya mafuta nchini Kenya imepanda tena
Bei ya mafuta nchini Kenya imepanda tena AFP - FRED TANNEAU
Matangazo ya kibiashara

Kila tarehe 14 ya kila mwezi, mamlaka hiyo hutangaza bei mpya ya mafuta. Mwezi huu, bei ya Super Petrol, imeaongezeka kwa Shilingi za nchi hiyo 3.40 kwa lita moja. 

Nayo bei ya mafuta aina ya Disel, imeongezeka kwa Shilingi 6.40 huku mafuta taa bei ikiongezeka kwa Shilingi 15.19 kwa lita. Kwa sasa, bei ya petroli jijini  Nairobi inauzwa kwa shillingi 182.70 

Mkurugenzi Mkuu wa EPRA Daniel Bargoria amesema kupanda kwa mafuta, kumechangiwa na kuongeza kwa gharama ya uigizaji na usafirishaji wa mafuta kutoka soko la kimataifa. 

Bargoria ametolea mfano uaangizwaji wa mafuta ya Super Petrol nchini Kenya kuongezeka kwa  8.63% mwezi Machi 2023. 

Aidha, ongezeko hili limekuja baada ya serikali kuondoa ruzuku kwenye diseli na mafuta  taa.  

Hatua hii inakuja wakati huu wananchi wa taifa hilo kubwa kiuchumi, likikabiliwa na kupanda kwa gharama ya maisha na ongezeko hilo, linatarajiwa kusababisha kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.