Pata taarifa kuu

"Yesu wa Tongaren” afikishwa mahakamani Magharibi ya Kenya

NAIROBI – Eliud Wekesa, maarufu kama  "Yesu wa Tongaren” raia wa Magharibi ya Kenya, amefikishwa mahakamani Alhamisi mjini Bungoma nchini Kenya, baada ya hapo jana kujiwasilisha kwa maofisa wa polisi kwa mahojiano na upelelezi zaidi baada yake kutakiwa kufanya hivyo. Hatua inayokuja wakati serikali ikiwa mbioni kuwadhibiti wahubiri wenye msimamo na itikadi kali.

Eliud Wekesa, maarufu kama  "Yesu wa Tongaren” raia wa Magharibi ya Kenya, anasema yeye ni Yesu na anamalaika wake
Eliud Wekesa, maarufu kama "Yesu wa Tongaren” raia wa Magharibi ya Kenya, anasema yeye ni Yesu na anamalaika wake © bbc
Matangazo ya kibiashara

Wekesa amejitangaza kuwa yeye ndiye Yesu ambapo pia ana malaika wake ambao anasema wanamsaidia katika kazi yake kama kristo mwana wa Mungu.

Polisi walimtaka kiongozi huyo wa dhehebu la New Jerusalem kufika mbele yao siku ya  Jumanne kuhojiwa kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka.

Kiongozi wa kidini raia wa Mji wa Bungoma Magharibi ya kenya kando na kuwa na malaika wake, pia na wanafunzi kumi na wawili kama ilivyokuwa katika Bibilia na wakati wa Yesu Kristo mwana wa Mungu.

Eliud Wekesa, maarufu kama  "Yesu wa Tongaren” amekuwa akisema kwamba yeye ni Yesu
Eliud Wekesa, maarufu kama "Yesu wa Tongaren” amekuwa akisema kwamba yeye ni Yesu © bbc

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari vya ndani, Wekesa amesema kuwa yeye hanatia yoyote ambayo imesababisha kutakiwa kuhojiwa na polisi. Amesisitiza kwamba yeye anafanya kazi ya kueneza injili kwa viumbe waliopotea.

Hatua ya kutakiwa kufika mbele ya polisi kwa kiongoizi huyo wa dini inakuja wakati huu maofisa wa usalama katika eneo la pwani ya Kenya wakiwa wanaendelea na zoezi la kufukua miili zaidi ya watu wanaodhaniwa kuwa walizikiwa baada ya kufairiki wakifunga kula kama walivyotakiwa na mhubiri wao Paul Makenzie.

Hapo jana Jumanne waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Kithure Kindiki, aliongoza awamu ya pili ya ufukuaji wa miili inayodaiwa kuzikwa katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya baada zoezi hilo kusitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Paul Mackenzie, 50, kiongozi wa dini nchini Kenya ambaye wafuasi wake walifariki baada yake kuwaagiza kufunga hadi wafe
Paul Mackenzie, 50, kiongozi wa dini nchini Kenya ambaye wafuasi wake walifariki baada yake kuwaagiza kufunga hadi wafe REUTERS - STRINGER

Waziri Kithure Kindiki alisema vifo vya watu hao ni uhalifu uliopangwa akieleza kuwa serikali itaweka wazi kilichotokea na kwamba tayari watu 25 wamekamatwa.

Aidha aliongeza kuwa maofisa wa upelelezi wanawafuatilia kwa karibu walioshirikiana na mhubiri Paul Mackenzie na uchunguzi unakaribia kukamilika.

Miili zaidi ya mia moja imefukuliwa katika shamba la Shakahola linalohusishwa na mchungaji Paul Makenzie
Miili zaidi ya mia moja imefukuliwa katika shamba la Shakahola linalohusishwa na mchungaji Paul Makenzie AP

Kuhusu ripoti ya uchunguzi wa kisayansi wa maiti zilizopatikana, waziri Kindiki alisema  kwamba wanafuatilia ripoti hiyo.

Katika hatua nyingine Watu wengine wawili waliokolewa siku Jumanne katika msitu huo na kufikisha idadi ya waliookolewa kuwa 65 katika oparesheni iliyofanywa na vitengo tofauti vya usalama nchini humo, idadi ya waliofariki ikifikiwa watu 133.

Polisi walifukua miili zaidi ya 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya
Polisi walifukua miili zaidi ya 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya AP

Rais William Ruto tayari ameunda tume ya uchunguzi kuchunguza vifo vya Shakahola katika kaunti ya Kilifi.

Katika hatua nyengine,  Paul Nthenge Mackenzie kiongozi wa dini aliyewaongoza wafuasi wake kufunga hadi wafe iliwamuone Mungu anatarajiwa kufikishwa tena mahakamni hii leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.