Pata taarifa kuu

Kenya: Mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie amefikishwa mahakamani

NAIROBI – Mhubiri mwenye utata nchini Kenya Paul Mackenzie ambaye alifika mbele ya mahakama mjini Malindi hii leo, atahukumiwa upya tena kwa tuhuma za ugaidi kufuatia mauaji ya wafuazi wake zaidi ya 100.

Mhubiri Paul Mackenzie amefikishwa mahakamani baada ya wafuasi wake zaidi ya 100 kufa baada ya kufunga kula chakula
Mhubiri Paul Mackenzie amefikishwa mahakamani baada ya wafuasi wake zaidi ya 100 kufa baada ya kufunga kula chakula REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Malindi katika kaunti ya Kilifi imemuachilia huru Mackenzie na washtakiwa wengine sita na kufunga mashtaka yanayowakilibili baada ya mahakama hiyo kusema haina uwezo wa kuwapa dhamana washukiwa hao. Ivy Wasike ni hakimu mkuu wa mahakama hiyo…

“Kwa washtakiwa nambari moja hadi Saba, hii file imewezwa kufungwa, na kuhusu swala la dhamana hii mahakama haina mamlaka ya kushughulikia swala hilo, na hili ombi la dhamana labda liwasilishwe kwa mahakama ya juu.” amesema Ivy Wasike hakimu katika mahakama ya Malindi.

Afisa kutoka ofisi ya mashtaka ya umma Vivian Kambaga amesema saba hao watafunguliwa mashtaka ya ugaidi katika mahakama ya Shanzu mjini Mombasa.

“Makosa yaliyodhirhirika kwa uchunguzi ni makosa ya itikadi kali chini ya kitendo cha kuzuia ugaidi.” ameelezaVivian Kambaga, Afisa kutoka ofisi ya mashtaka ya umma nchini Kenya.

Baada ya mahakama kukamilisha shughuli zake, Mackenzie na wenzake walikamatwa nje ya jengo la mahakama hiyo na maafisa kutoka kitengo cha GSU. Mackenzi alikuwa na haya ya kusema.

“Uamuzi sioni kama kuna shida isipokuwa sasa nimezuiliwa tu bado, kwa hivyo bado haijabadilisha kitu.”amesema Paul Makenzie.

Baadhi ya familia ya wafuasi wa mhubiri huyo walikuwa na maoni mbalimbali...

Nilikuwa naomba kwamba tafadhali serikali kama inawezekana for the first time, naomba haki itendeke, sheria itendeke.Mfuasi wa mhubiri Paul Makenzie

Naona hapo kwamba wamefanya jambo la maana kwa sababu mashtaka yameongezeka. Tuwapate wapendwa wetu wazima ama wamekufa.”Mfuasi wa mhubiri Paul Makenzie.

Tayari watu 109 wameripotiwa kufa katika eneo la Shakahola baada ya kufunga kula chakula wakiwa na matumaini ya kumuona Yesu Kristo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.