Kenya: Rais Ruto atoa wito wa kushtakiwa kwa mhubiri mwenye imani potofu
NAIROBI – Rais wa Kenya William Ruto ametoa wito wa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa Paul Mackenzie mchungaji wa kanisa anayekabiliwa na utata baada ya wafuasi wake zaidi ya 40 kufariki wakisusia kula.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mackenzie anadaiwa kuwaagiza wafuasi wake wa kanisa la Good News International pwani ya Kenya, kutokula chakula hadi wafariki akiwahidi kuwa hiyo ingekuwa njia rahisi ya kukutana na Yesu Kristo kwa haraka.
Rais Ruto katika taarifa yake amemtaja mchungaji huyo kama mtu gaidi anayestahili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wito wa rais Ruto unakuja wakati huu ambapo pia, raia na mashirika ya kutetea haki za binadamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki wakiishinika serikali kumchukulia hatua kali mchungaji huyo kutokana na imani yake ya kupotosha raia.
Kauli ya mkuu wa nchi ikija muda mfupi baada ya Polisi kupata mwili mitatu zaidi kutoka kwenye kaburi la pamoja karibu na mji wa pwani wa Malindi. Hii inafikisha idadi ya waliofariki kufika watu 42.
Maafisa wakuu wa usalama wakiongozwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome na mkurugenzi mkuu wa idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai Mohamed Amin wakitarajiwa kujiunga na kikosi cha wachunguzi katika eneo Shahola palipopatikana makaburi hayo.
Wafuasi wa mchungaji wa mchungaji Paul Mackenzie waliaamini kuwa iwapo wangefariki kutokana na njaa basi wangekutana na kristo kwa haraka.