Pata taarifa kuu

DRC: Raia wilayani Masisi wanaishi kwa mashaka licha ya M23 kuondoka

NAIROBI – Wakaazi wa kijiji cha MOSHAKE wilayani Masisi, Mashariki mwa DRC wanasema bado wanaishi kwa mashaka licha ya kuondoka kwa waasi wa M 23, kwa sababu wanaendelea kusumbuliwa na makundi mengine ya waasi.

Wanajeshi wa EAC waliotumwa nchini DRC kulinda usalama wa raia
Wanajeshi wa EAC waliotumwa nchini DRC kulinda usalama wa raia AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Hili limebainishwa na Mwandishi wetu Chube Ngorombi, alipozungumza na raia hao, wakati wa ziara ya kikosi cha Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki, linalotembelea maeneo ambayo waasi wa M 23 wameondoka.

Waasi wa M23 walitakiwa kuondoka katika maeneo wanayoshikilia mashariki ya DRC kwa mujibu wa makubaliano ya Luanda Angola na kukabidhi sehemu hizo kwa vikosi vya Jumuiya ya Afrika mashariki.

Licha ya hatua hiyo ya kuondoka kwa waasi hao, baadhi ya raia wanahisi kuwa waasi hao wanaondoka kwa kasi ya pole pole kinyume na ilivyotarajiwa.

Hawa hapa ni baadhi ya raia waliozungumza na mwandishi Chube Ngorombi.

“Hapa waasi ukiwa na kitu wanachukua kwa nguvu wanaua watu wengine ndio kile kinasababisha watu wanakimbia.” Amesema mmoja wa raia wa Moshake aliyezungumza naye mwandishi wetu Chube Ngorombi.

01:08

Raia wa Moshake katika Wilaya ya Masisi nchini DRC

Baadhi ya raia waliotoroka makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa na makundi hayo ya waasi kwa sasa wameanza kurejea katika makazi yao wakiwa na matumaini ya kurejelea maisha yao ya awali kabla ya kutatizwa na makundi ya watu wenye silaha.

Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wao wamewahakikishia raia wa maeneo hayo ulinzi na usalama haswa wakati huu kukiwepo na hofu ya makundi hayo ya waasi kurejea baada ya wanajeshi hayo kuondoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.