Pata taarifa kuu

Kenya: Mahakama kusikiliza kesi dhidi ya kampuni ya Meta

NAIROBI – Mahakama nchini Kenya, imeamua kuwa ina uwezo wa kusikiliza kesi dhidi ya kampuni ya Meta, iliyoshtakiwa kwa kuwafuta kazi zaidi ya wafanyakazi 200 wanaofanya kazi na mtandao wa facebook.

Kampuni ya Meta
Kampuni ya Meta REUTERS - DADO RUVIC
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo iliwasilishwa na wafanyazi wa Facebook 183 wanaofanya kazi jijiji Nairobi, tarehe 17 mwezi Machi, kulalamikia kufutwa kazi kinyume cha sheria.

Kabla ya uamuzi huo, Mawakili wa Meta walisema Mahakamama hiyo ya ajira nchini Kenya, haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo dhidi ya kampuni hiyo, makao yake makuu hayapo Kenya.

Aidha, walikuwa wamejitetea kuwa wafanyazi hao hawakuwa wameajiriwa na Meta ambayo pia inamiliki mitandao ya kijamii ya Instagram na WhatsApp.

Hata hivyo, Jaji Mathews Nduma Nderi ametupilia mbali uetetezi wao na kusema Mahakama ina uwezo wa kusikiliza na kuendelea na kesi hiyo.

Mbali na kesi hiyo kampuni hiyo inakabiliwa na kesi nyingine nchini Kenya ambapo shirika moja lisilo la kiserikali na raia wawili wa Ethiopia wameishtaki kwa kushindwa kudhibiti kauli za uchochezi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.