Pata taarifa kuu

DRC: Maiti ya watu zaidi ya 30 yagunduliwa kusini mgharibi wa Bunia

NAIROBI – Mashariki mwa DRC hapo jana Jumatano kuligunduliwa maiti za watu zaidi ya 30 wanaodaiwa kuwa waliuawa katika kijiji cha Mungamba na maeneo jirani, umbali wa kilomita 100 kusini mgharibi mwa jiji la Bunia mkowani Ituri.

Ramani ya DRC
Ramani ya DRC RFI/Anthony Terrade
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yanadaiwa kutekelezwa siku ya Jumatatu ya wiki hii, duru za kiusalama zikiwatuhumu waasi ADF na washirika wao kwa kuhusika.

Mashambulio hayo yalitekelezwa katika vijiji vinne, kikiwemo kile cha Palipopo. John Kihimba ni makaazi Wilayani Mambasa.

"Watu kadhaa waliuawa kwa Malanga, sisi kwa upande wetu tuahisi kwamba muda wa dharura uko kwatesa raia wala sio kuwalinda na kuwatetea.” ameeleza John Kihimba ni makaazi Wilayani Mambasa
00:08

John Kihimba ni makaazi Wilayani Mambasa

Baadhi ya wahanga wameripotiwa kukatwa vichwa wakati wa tukio hilo, mali ya thamana isiojulikana pamoja na mifugo zikiporwa. Kanali Mak Hazukay ni msemaji wa opereseheni Shujaa.

“Inawezekana kuna waasi wachache sehemu fulani hivi punde tutawatokomeza.” Kanali Mak Hazukay ni msemaji wa opereseheni Shujaa
00:19

Kanali Mak Hazukay ni msemaji wa opereseheni Shujaa

Mauji haya mpya, yametokea wakati huu wakuu wa jeshi la FARDC na UPDF wakiwa katika ziara mjini Beni, kuangazia uwezekano ya kupanua opersheni shujaa kote Ituri na Beni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.