Pata taarifa kuu

DRC: Wakazi wa Kivu kaskazini walaumiwa kwa kushirikiana na waasi wa ADF

NAIROBI – Gavana wa Jimbo la Kivu kaskazini Luteni jenerali Constat Ndima amewalaumu baadhi ya wananchi wa mji wa Beni kwa kushirikiana na waasi wa ADF na kuwataka watambuwe kwamba swala la Amani ni swala la wananchi wote.

Baadhi ya raia wa Kivu kaskazini wametuhumiwa na walinda usalama kwa kushirikana na makundi ya waasi
Baadhi ya raia wa Kivu kaskazini wametuhumiwa na walinda usalama kwa kushirikana na makundi ya waasi © Sebastien Kitsa Musay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Lengo hasa lilikuwa kudhibiti ghasia za waasi waliokimbia katika majimbo hayo mawili kwa kuweka tawala za kijeshi na kuimarisha operesheni za usalama.

Lakini wananchi na wadau mbalimbali wamekuwa wakiikosoa hatua hiyo ambayo wanaona kwa asilimia kubwa haijafaanikiwa, kutokana na kuendelea kwa mauaji.

Francois Alwende mchambuzi wa siasa za DRC hapa anaangazia suala hili

" Nadhani kwamba hilo sio jambo la kwanza kwa viongozi wa DRC kuzungumzia swala la baadhi ya raia kwa DRC  kushirkiana na waasi na ni jambo ambalo linajulikana kwa mtu yeyote aliye katika siasa."ameeleza Francois Alwende mchambuzi wa siasa za DRC.

Uasi wa Vuguvugu la Machi 23 (M23) huko Kivu Kaskazini umeongeza mambo zaidi huku rasilimali zikielekezwa kinyume na uvamizi huo.

Kinshasa imeendelea kuituhumu jirani yake Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaoendelea kuhangaisha usalama wa raia katika êneo la mashariki kwa muda sasa.

Tayari wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki wametumwa nchini DR Congo kama njia ya kuwalinda na kuwakinga raia kutokana na mashambulio yanayotekelezwa na waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.