Pata taarifa kuu

Marekani imezitaka Rwanda na DRC kuacha kushirikiana na waasi

NAIROBI – Nchi ya Marekani, kwa mara nyingine imezitaka nchi za Rwanda na DRC kuacha kushirikianana makundi yenye silaha, kwani kufanya hivyo kunahatarisha usalama na ustawi wan chi za ukanda.

Rais Felix Tshisekedi wa DRC na  Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Felix Tshisekedi wa DRC na Paul Kagame wa Rwanda. © afp:Tchandrou Nitanga
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa, mwakilishi wa marekani kwenye umoja huo anayehusika na masuala ya kisiasa, Robert Wood, amesema ni lazima nchi hizo ziache kutuhumiana na badala yake kusitisha ushirikiano wao na makundi ya M23 na FDLR.

“Marekani inasisitiza wito wake kwa Rwanda kuacha kuunga mkono M23 ambao wameekewa vikwazo na UN, tunawataka wanachama wa baraza hili kuwazia namna ambavyo uungwaji mkono wa namna hii unakwenda kinuyme na vikwazo vilivyotangazwa.“amesema Robert Wood.

00:28

Robert Wood kuhusu Rwanda na DRC

Kinshasa imekuwa ikiituhumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 madai ambayo Rwanda imeendelea kukanusha.

Kwa upande mwengine, ghasia za kijamii zinazoendelea magharibi mwa nchi hiyo zimesababisa watu 300 kupoteza maisha tangu mwezi Juni 2022, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema katika ripoti iliyotolewa leo Alhamisi.

Vurugu hizo zilianzia kwenye mgogoro wa ardhi kati ya Wateke wanaojinasibu kuwa ni wazawa na wamiliki wa vijiji vilivyopo kando ya mto Kongo umbali wa takribani kilomita 200 na Wayaka waliokuja kuishi baada yao.

Matamshi ya Marekani yanakuja wakati huu ambapo  kundi la waasi wa M23 lilitakiwa  kuwa limejiondoa kwenye maeneo wanayoyakaliwa mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, bado wameendelea kuonekana.

Licha ya uwepo wa makubaliano ya hatua za kuchukua kumaliza mzozo unaoendelea ikiwemo usitishaji wa mapigano ambao umeshindwa kuheshimiwa, ndivyo ilivyo kwa agizo la waasi hao kuondoka kwenye maeneo wanayoyakalia ifikapo hivi leo, jambo ambalo sasa ni wazi halitatekelezeka

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.