Pata taarifa kuu

DRC: CODECO watuhumiwa kuwaua watu 20 katika kijiji cha Petsi

NAIROBI – Waasi wanaoaminiwa kuwa ni wa CODECO, wameua watu wanaokadiriwa kufikia 20 katika kijiji cha Petsi, siku moja baada ya kuwateka kwenye mji wa bambou, wilayani Djugu mkoani Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

Waasi wa kundi la CODECO wametuhumiwa kwa mauaji ya watu 20 nchini DR Congo
Waasi wa kundi la CODECO wametuhumiwa kwa mauaji ya watu 20 nchini DR Congo AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Antony Mwalusyia, ni msamaji wa jeshi la Congo. 

"Magaidi 20 wa ADF waliuawa katika mapambano yaliohusishwa waasi wa jeshi la taifa katika makabiliano yalioendelea kwa zaidi ya nusu saa."ameeleza Antony Mwalusyia, msamaji wa jeshi la Congo. 

00:29

Antony Mwalusyia, msamaji wa jeshi la Congo

Makundi ya waasi yamekuwa yakiripotiwa kuwashambulia raia katika eneo la mashariki ya DRC kwa muda sasa wakati huu vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki vikitumwa katika eneo hilo la nchi kuwalinda raia kutoka kwa mashambulio ya waasi.

DRC imeendelea kuituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 madai ambayo Kigali kwa upande wake imeendelea kukanusha.

Hivi majuzi wajumbe wa baraza la usalama katika umoja wa mataifa walizuru DRC kutathmini hali ya usalama katika eneo la mashariki.

Maelfu ya raia mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameripotiwa kuyahama makazi yao kwa kuhofiwa kushambulia na makundi ya watu wenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.