Pata taarifa kuu

Msaada zaidi wa Kibinadamu wawasili DRC

NAIROBI – Tani 35 ya msaada wa kibinadamu unawasili leo asubuhi mjini Goma, Mashariki mwa DRC kuwasaidia maelfu ya wakimbizi waliokimbia makaazi yao kutokana na vita kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali.  

European commission aid continues to arrive in DRC
European commission aid continues to arrive in DRC © EU
Matangazo ya kibiashara

Msaada huo  kutoka Umoja wa Ulaya, unatarajiwa kuwafikia watu 800,000 ambao wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu tangu kuanza kwa vita hivyo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. 

Huu utakuwa ni msaada wa pili, baada ya EU kutuma msaada wa kwanza Machi 10, siku chache baada ya rais wa Ufaransa kutembelea nchi hiyo na kuahidi kuwa mataifa ya Ulaya yangetuma msaada huo. 

Miongoni mwa misaada hiyo ni pamoja na vifaa vya kutoa huduma za afya, chakula, mahema na mablanketi kwa ajili ya wakimbizi wanaohangaika.  

Umoja wa Ulaya unasema msaada huu umegharimu karibu Euro Laki nne.  

Kwa ujumla mataifa ya EU yametenga Euro Milioni 47 kuwasaidia raia waliothiriwa na vita hivyo.  

Haya yanajiri wakati huu ripoti ya umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumatano ya wiki hii inaonesha kuwa zaidi ya watu laki 1 wamekimbia makazi yao na wengine mamia wameuawa kutokana na mashambulio ya makundi ya waasi jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Akinukuu ripoti ya ofisi ya misaada ya kibinadamu, msemaji wa umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema zaidi ya watu elfu 50 wamekimbia makazi yao kwenye mji ya Rutshuru na kuomba hifadhi Kibirizi.

Aidha watu wengine elfu 55 kutoka eneo la Masisi, walikimbilia vijiji jirani na kwenye mji wa Goma na ule wa Minova jimboni Kivu Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.