Pata taarifa kuu

Wanawake wanavyopigania haki yao ya kilimo cha wimbi kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi

Huku Ulimwengu mzima ukikabiliwa na athari ya mabadiliko ya tabia nchi,wanawake kaunti ya Bomet nchini Kenya wapo kwenye hatari ya kupoteza kitega uchumi kubwa ambacho ni uzalishaji wa wimbi. Wanalazamika kubadili mbinu ya kilimo hiki, ili kuendelea kupata mapato na haki ya kiuchumi, kutoka kwa kilimo hicho cha Wimbi na kumudu hitaji kubwa ya zao hilo kutokana na ongezeko la wagonjwa wa kisukari.Carol Korir amezuru kaunti ya Bomet na kutuandalia ripoti ifuatayo.

Bi Nancy Rono mkulima wa Wimbi kaunti ya Bomet nchini Kenya
Bi Nancy Rono mkulima wa Wimbi kaunti ya Bomet nchini Kenya © Carol Korir
Matangazo ya kibiashara

Ni alasiri siku ya Jumamosi,katika kijiji cha Tarakwet ,kaunti ndogo ya Sotik ,iliyoko kusini mwa bonde la ufa. Boma kwake  Jannifer Birir ,wajukuu wanacheza  wakingalia mifugo yake ya kondoo.

Jannifer ,amekuwa akimhudumia mamake mzazi anayeugua kisukari,anaelezea ugumu anaopata kumhudumia.

Ukiwa na mgonjwa wa kisukari huwezi kuenda popote ,kazi ni kumhudumia,kila saa anasema ana njaa,na wakati kama huu wa kiangazi  ,ana shida,hakuna kitu shambani,mahali huwa tunapata pesa,hakuna,”alielezea.

“ Na ukienda hospitali kwa vipimo daktari anakupangia ,mgonjwa lazima apate chakula kila mara,ugali na uji wa wimbi,”alisema Janiffer.

Hao ni baadhi ya wanawake wanaolima wimbi,masaibu yao si tofauti

“Hatupati mbegu ya wimbi kwa urahi si,tena kuna hatari ya ukame,mwaka huu wa 2023,hakuna mvua na wimbi inaweza kukauka ,”alisema Emmah Langat mmoja wa wakulima.

“  Tunaenda mbali kutafuta mbegu na tukipata,ni bei ghali,tena kuna hatari ya ugonjwa ambao kikwetu wanaita ‘chelalit’ hapo iko shida,”alisema Rachel mkulima mwingine.

Taasisi ya utafiti wa kilimo na ufugaji nchini Kenya , KALRO, imesikitika  kuhusu kushuka kwa uzalishaji wa chakula hiki chenye lishe,na wanashauri wakulima hao kubadilisha mfumo.Dr Eliud Kiregler ni mkurugenzi wa taasisi hiyo.

“Upungufu wa uzalishaji wa wimbi ,moja ya sababu ni kuwa wakulima wanaamini lazima utumie kipande cha ardhi ambacho hakijawahi kutumika,sasa kuna uhaba wa mashamba,huwezi kuwa kila mara unakuwa na kipande kipya upande wimbi,”alisema Daktari Eliud Kireger.

Tumemtembelea Nancy Rono,katika kijiji cha Kamureito , Mmoja  wa wale ambao wamekumbatia kilimo cha kisasa kutumia mistari baadala ya kusambaza kiholela.

“ Kwa laini ni sentimeta thelathini hadi kwa laini,kwa kipande hiki naweza nikavuna hadi magunia manne ,zamani ningepata gunia moja,wajua hii wimbi hata mume wako hawezi kukuliza pesa umetoa wapi,ni pesa ya wanawake,”alisema Nancy Rono alivyokuwa akituonesha namna anavyofanya kilimo chake.

Joel Korir ni mtaalam wa kilimo aliyestaafu.  Kwa sasa anafanya kazi kama mshauri wa kijamii.

“  Unajua ukipanda kwa laini hata ni rahisi kwa wazee,unaweza ukamchukua mzee wako mkapalilia pamoja, badala ya kwenda naye kuinama kungoa magugu,”alisema Joel Korir.

Katika kilimo cha zamani  cha wimbi,wanawake walitumia ardhi ambayo haijawahi kutumika ,kuchoma udongo ,kilimo ambacho kwa s asa hakiwezekani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.