DRC: Wakimbizi waandamana Goma wakitaka chakula
NAIROBI – Polisi jijini Goma wamewatawanya raia hao walioandamana wakilalamikia mateso wanayoyapitia kambini bila ya kupata msaada. Raia huyu wa Goma ni miongoni mwa walioandamana
Imechapishwa: Imehaririwa:
Raia wa Goma
“Watoto wana njaa na Sisi hatuna hata pesa ya kununua chakula, ombi letu nikupata haki yetu ya kupata chakula kama sivyo waturejeshe kwetu ambako kuna waasi wa M23.”amesema raia wa Goma.
Watetezi wa haki za binadamu pamoja na baadhi ya raia hao walioandamana wamesema kutokana na changamoto wanazozipitia zimesababisha baadhi yao kuamua kurejea katika vijiji vyao vya kawaida wilayani Masisi na Rutshuru, licha ya ukosefu wa usalama vijijini mwao.
Bose Bamwe jean Étienne ni mtetezi wa haki za binadamu kutoka shirika la Acadepa wilayani nyiragongo.
Bose Bamwe jean Étienne ni mtetezi wa haki za binadamu Goma
“Imepita sasa zaidi ya miezi miwili bila kupata msaada wa chakula,tunataka serikali yetu na wahusika wa masuala ya kijamii kusaidia watu hawa walio hatarini.”amesemaBose Bamwe jean Étienne ni mtetezi wa haki za binadamu kutoka shirika la Acadepa wilayani nyiragongo.
Nzangi Butondo ni waziri anayehusika na masuala ya elimu na vyuo vikuu nchini Congo DR.
Nzangi Butondo
“inabidi serikali ipange vizuri huduma ya kugawa misaada ilipasitokee tena shida.”amesema Nzangi Butondo
Haya yanajiri wakati huu waasi wa M23 wakiendelea kushutumiwa kwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia wa eneo la mashariki.