Pata taarifa kuu

Mombasa kama historia muhimu ya Kenya

Mombasa iliyo sehemu ya Pwani ya Kenya huenziwa kutokana na ukaribu wake na bara hindi na iliyo na historia muhimu kuhusu Kenya

Mmoja wa Mwanzilishi wa mgahawa wa Forodhani  jijini Mombasa,Abdulhamid Dor. Forodhani ilikuwa sehemu ya bandari ya zamani
Mmoja wa Mwanzilishi wa mgahawa wa Forodhani jijini Mombasa,Abdulhamid Dor. Forodhani ilikuwa sehemu ya bandari ya zamani © Carol Korir
Matangazo ya kibiashara

 

Jiji la Mombasa,ni jiji muhimu la kihistoria nchini Kenya ambapo utawala wa Kikoloni ulianzia ,ukiwa ni jiji kuu hadi mwaka wa 1906 .Ulishuhudia utawala wa Sultana,Wareno ,Waomani na hatimaye wa Uingereza ambao ndo ulihamisha makao makuu yake hadi Nairobi.Carol Korir kwenye msururu wa ripoti tofauti kuhusu mji huo  ,anatutambulisha kuhusu jiji hili la Kale kwenye ripoti ifuatayo. 

Dakika chache kabla saa kumi na moja ,mji wa Mombasa huamka kwa sauti za  ndege kwenye maeneo yenye miti ya miembe na mnaza pia Mwadhini ,idadi kubwa ya wakaazi wakiwa wanaelekea msikitini kwa swala la alfajiri. 

Na  sauti zingine ambazo huweki kukwepa unapokaribia maeneo ya barra barra ,ni sauti za  Tuk Tuk ambazo zinatumika sana kwa usafiri. 

Tayari kujiandaa kwa shughuli za siku ni akina mama ambao ni wapishi ,tayari kukuhudumia kwa mapochopocho mbali mbali anavyonielezea Maimuna Errey mmoja wa wapishi kiboko. 

“ Mombasa kuna joto ,Pwani yetu hii kwa hivyo juisi ya Ukwaju ni burudani tosha.Unachemsha maji yako na ukwaju pamoja na iliki ,unaongeza tena maji ukishavuruga “,alisema Maimuna. 

Anaongezea kuelezea kuhusu mapishi, “Mapishi ya Pwani utaskia watu wanayasifu kwa sababu una viungo vingi tunaweka madoido ,vinakuwa na ladha yaani vyakula vinavutia kwa macho na hata kula. Asubuhi unaamka ukishajua nini unapika kwa mfano kama ni pilau unaona mimi nishachemsha nyama yangu ya mbuzi,”alielezea Maumuna Errey. 

Na ukiwa hujafika maeneo ya Ferry inayounganisha kisiwa cha Mombasa na Pwani ya Kusini ,hujafika. 

Sehemu  pambe ya kula ni mgahawa wa Forodhani ambayo ilikuwa sehemu ya bandari ya zamani .Abdulamid Dor ni moja wa  mwanzilishi   

“Ilikuwa kama bohari lakini halikuwa limetumika kwa muda mrefu, katika kutafuta tafuta tukafuatilia kuona tunaweza kufanya mgahawa,kwenye uanzilishi ,palijulikana kama ‘ go down’ tulikuwa tukisema tunaenda ‘go down’,maanake tulikuwa tukikaa, ahh mwaenda wapi ,twaenda go down”. 

“ Hapa tunakaa kwenye maji,nimetumia karibu magurudumu 1200 ya malori ,nilikuwa najaza ili kuzuia maji,”alisema Dor. 

Mombasa hupokea watalii wengi kila mwaka wanaozuru kufurahia bahari ya Hindi,Mapishi na kujifundisha historia na tamaduni .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.